Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 02:23

Wizara ya Sheria Marekani yataka mahakama ya Juu kukataa ombi la Trump la nyaraka za siri


FILE - Rais wa zamani Donald Trump
FILE - Rais wa zamani Donald Trump

Wizara ya Sheria ya Marekani Jumanne imeitaka Mahakama ya Juu kukataa ombi la Rais wa zamani Donald Trump kumpa uwezo tena wa kisheria msuluhishi wa kujitegemea kuzitathmini nyaraka za siri zilizokamatwa kutoka katika makazi yake ya Florida.

Hatua hii ikiwa ni sehemu ya mapambano yake ya kisheria dhidi ya wachunguzi wanaoangalia Rais Trump alivyoshughulikia rekodi nyeti za siri za serikali.

Rais wa zamani Trump alifungua maombi ya dharura Oktoba 4, akiwataka majaji kuondoa uamuzi wa mahakama ya chini kumzuia asiwepo msuluhishi huyo, anayejulikana kama msimamizi maalum, kuzipitia zaidi ya nyaraka 100 zilizokuwa na alama ya siri ambazo ni kati ya takriban nyaraka 11,000 zilizokamatwa na maafisa wa FBI katika makazi yake ya Mar-a-Lago huko Palm Beach Agosti 8.

Katika kuwasilisha Jumanne, Wizara ya Sheria ilisema ombi la Rais wa zamani Trump likataliwe kwa sababu hakuweza kuonyesha “makosa ya wazi” yoyote katika uamuzi uliotolewa na mahakama ya chini, au vipi itamuathiri.

Rais wa zamani Trump alikwenda mahakamani Agosti 22 ili kutaka kuizuia Wizara ya Sheria isipate fursa ya kuziangalia nyaraka wakati inaendelea kufanya uchunguzi wa kihalifu kwa Trump kushikilia nyaraka za serikali, baadhi zikiwa zimewekewa alama ya rekodi nyeti sana zikiwemo za siri ya juu kabisa, huko Mar-a-Lago baada ya kuondoka madarakani Januari 2021.

Nyaraka nyeti zilizokamatwa na Shirika la Upelelezi wa Makosa ya Jinai FBI katika makazi ya Rais wa zamani Donald Trump, Florida.
Nyaraka nyeti zilizokamatwa na Shirika la Upelelezi wa Makosa ya Jinai FBI katika makazi ya Rais wa zamani Donald Trump, Florida.

Wakati huo Trump alimuomba jaji kumteua msimamizi maalum, baadaye jaji alifanya hvyo, kuzitathmini nyaraka hizo na kuzipitia kuona iwapo yoyote inaweza kuwa ni haki yake kuwa nayo na uwezekano wa kutopewa wachunguzi.

Mahakama ya Juu hiyo yenye uwiano wa majaji wa kikonsavativ waliowengi 6 -3 kati yao watatu wameteuliwa na Trump.

Mahakama ya Rufaa ya 11 ya Marekani iliyoko Atlanta Septemba 21 ilizuia uamuzi wa Jaji wa Wilaya Aileen Cannon, ambaye anasikiliza kesi ya Trump.

Cannon alizuia kwa muda Wizara ya Sheria ya Marekani kuzichunguza nyaraka zilizokamatwa mpaka pale msimamizi maalum aliyemteua, Jaji Raymond Dearie, azitambue nyaraka zozote ambazo zitaonekana kuwa ni haki ya Trump kuwa nazo.

Cannon alimtaka Dearie kupitia nyaraka zote zilizokamatwa, ikiwemo zile nyeti, ili kutambua chochote ambacho kinaangukia chini ya siri kati ya wakili na mteja wake au upendeleo wa kiutendaji, nadharia ya kisheria ambayo inalinda baadhi ya mawasiliano ya White House kutowekwa hadharani, na hivyo ni katazo pia kwa wachunguzi.

Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la Reuters.

XS
SM
MD
LG