Miongoni mwa walioripotiwa kupokea wito huo wa mahakama ni Dan Scavino, mkurugenzi wa zamani wa mitandao ya kijamii wa rais huyo wa zamani, na Bernard Kerik, kamishna wa zamani wa polisi wa Jiji la New York, ambaye alichochea madai ya udanganyifu wa wapiga kura katika uchaguzi wa rais wa 2020 pamoja na meya wa zamani wa jiji la New York Rudy Guiliani, pia mshirika wa karibu wa Trump kwa muda mrefu. Gazeti la Times linaripoti idadi ya washauri wengine wakuu na wasaidizi wa ngazi ya chini pia walipokea wito.
Wito huo wa mahakama unalenga kupata taarifa kuhusu jarinbio lililoshindwa la Trump na washirika wake la kutengua matokeo ya uchaguzi wa 2020 kwa kuwasilisha orodha mbadala za wapiga kura wa uwongo kutoka baadhi ya majimbo.