Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 05:37

Biden abainisha vitisho vya demokrasia Marekani


Rais Joe Biden akizungumza nje ya Ukumbi wa Uhuru, Alhamisi, Septemba 1, 2022, huko Philadelphia. (Picha ya AP/Evan Vucci).
Rais Joe Biden akizungumza nje ya Ukumbi wa Uhuru, Alhamisi, Septemba 1, 2022, huko Philadelphia. (Picha ya AP/Evan Vucci).

Rais Joe Biden  alitumia neno “demokrasia” mara kadhaa katika hotuba yake iliyokuwa na hisia  kwa kile alichokiona ni jambo hatari sana wakati ambalo Marekani inakabiliwa nalo kwasababu ya Trump na warepublican wanasema kuwa anabainisha vitisho vya demokrasia ya Marekani.

Rais Joe Biden alitumia neno “demokrasia” mara kadhaa katika hotuba yake iliyokuwa na hisia kwa kile alichokiona ni jambo hatari sana wakati ambalo Marekani inakabiliwa nalo kwasababu ya Trump na warepublican wanasema kuwa anabainisha vitisho vya demokrasia ya Marekani. Biden alielezea bayana nani anadhani anahusika na hilo.

Marekani iko katika kipindi hatari sana, Rais Joe Biden anaamini. Alhamisi usiku, alielekeza lawama kwa mtu mmoja.

“Hakuna swali kwamba chama cha Republican hivi leo kinatawala, kinasukumwa na kunyanyaswa na Donald Trump na Warepublican wanaojiita MAGA. Hilo ndiyo tishio la nchi yetu,” amesema Rais Biden.

Biden alizungumza kwa dakika 25, na wakati huo, alisema neno moja siyo chini ya mara 25, nalo ni Demokrasia.

Alilitumia neno hilo dhidi ya warepublican walioelemea kwa Trump ambao walikuwa wakiunga mkono madai ya Trump yasiyo ya kweli kwamba uchaguzi wa mwaka 2020 uliibiwa, ambao wanajitahidi kukandamiza wapiga kura katika majimbo muhimu, na ambao walishiriki au kushawishi jaribio la uasi katika jengo la Capitol Januari 6 mwaka 2021.

Lakini pia Biden alitumia neno hilo kuashiria kile anachoamini ni mustkabali mzuri wa baadaye, kukionga chama chake – ambacho hivi karibuni kilipata mafanikio na kujigamba huo ndiyo ushahidi.

Rais Biden anasema “Tunaweza kuchagua njia ya kusonga mbele kuelekea siku za usoni. Huko mbele kwenye uwezekano wa kujengandoto na matumaini, na sisi tuko katika njia hiyo ya kusonga mbele.”

Katika majibu ya kupinga hotuba hiyo, kiongozi wa Republican katika bunge Kevin McCarthy alimshutumu Biden kwa mgawanyiko.

“Rais alipozungumza usiku kwenye Independence Hall, mistari ya kwanza ya maneno yaliyotoka kinywani mwake ni vyema aombe msamaha kwa kukashifu mamilioni ya wamarekani kuwa na wafashisti.”

Hii ni ziara ya pili ya Biden katika jimbo Keystone wiki hii. Pennyslvania ni jimbo lenye ushindani katika kile ambacho kitabainisha ni eneo la mapambano kati ya wademocrat wa Biden na warepublican wa Trump katika uchaguzi wa katikati ya muhula baadaye mwaka huu.

Mapema japa, msemaji wa White House Karine Jean-Pierre alisistiza kuwa hii ilikuwa ni zaidi ya hotuba tu. “Ni kuhusu mapambano ya kimsingi kote ulimwenguni kati ya utawala wa kiimla na demokrasia na jinsi demokrasia ilivyo msingi muhimu kwa nchi hii kusonga mbele.”

Wachambuzi wanahoji hilo, wakati ushindi wa karibuni wa Biden katika sheria na vipaumbele vinavyoingiliana na ujumbe wa hotuba yake.

William Howell, wa Chuo Kikuu cha Chicago) anasema “tunaanza kuona masuala gani ambayo wademocrat wanayaona kuwa ni fursa nzuri: bunduki ni moja wapo, demokrasia ni jingine. Inafurahisha, pia kwamba hakuelezea zaidi suala la kisheria katika hayo. Na bado hayo ndiyo aliyazungumzia, lakini siyo kwa jicho la kupitisha sera hivi sasa lakini kwa jicho ya kuelekea kuwepo na mabadiliko katika Bunge.”

Wanahistoria ambao wanafuatilia matamshi ya rais wanasema sauti ya Biden ilionekana imebadilika kuelekea upigaji kura wa mwezi November wakati muda huo ukiwa unakaribia.

Naye Jeremi Suri, wa Chuo Kikuu cha Texas, Austin anaelezea

Naamini kuwa matamshi makali kutoka kwa rais na wademocrat wengine yanafanya kazi. Kuna usahidi kwamba wapiga kura huru – siyo wapiga kura wa Trump, wapiga kura wengi huru—hasa wanawake, hata katika majimbo ya waconservative, kama vile Texas na Kansas, wamechoshwa na uingiliaji kati wa warepublican. Na kweli kabisa, wamechoshwa na habari za kuvunja sheria kulikofanywa na rais wa zamani. Habari nyingi kuhusu Trump, inawafanya wademocrat waonekane vizuri”

Lakini jana usiku huko Philadelphia, rais alisema neno moja kura mara nane. Badala ya kuonyesha picha ya Amerika anayoiona yeye.

“Sisi ni Marekani, Marekani. Tunamuomba mwenyenzi mungu alilinde taifa hili na wale wanaosimama kuiangalia demokrasia yetu. Nyote namuombea mwenyenzi mungu awalinde. Demokrasia. Shukran,” Rais Biden amesema.

Ni upande gani utaibuka na ushindi wakati wamarekani watakapotumia haki ya kidemokrasia mwezi Novemba?

XS
SM
MD
LG