Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Novemba 22, 2024 Local time: 22:51

Rais wa zamani Trump akana mashtaka 34 dhidi yake mahakama ya New York


Former U.S. President Trump indicted by Manhattan grand jury, in New York City
Former U.S. President Trump indicted by Manhattan grand jury, in New York City

Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump Jumanne amekana makosa katika mahakama ya jimbo la New York kuhusu mashtaka 34 yaliyofunguliwa yakimshutumu kughushi rekodi za biashara kwa kuendeleza uhalifu ambao haukutajwa – ulioelezwa na waendesha mashtaka katika juhudi ya kuficha malipo ya kumnyamazisha mcheza filamu za ngono ili imsaidie kushinda urais mwaka 2016.

Katika kesi ya kwanza ya jinai kuwahi kufanyika dhidi ya kiongozi wa sasa au wa zamani wa Marekani, Mwendesha Mashtaka wa Manhattan Alvin Bragg alidai katika “taarifa ya vithibitisho” vilivyoambatana na mashtaka hayo kuwa Trump “alirejea mara kadhaa na kufanya wizi wa udanganyifu katika rekodi za biashara ili kuficha vitendo vya uhalifu vilivyoficha taarifa inayomchafua kuwafikia wapiga kura wakati wa uchaguzi wa urais 2016.

Ikiwa ni sehemu ya mpango huo, kulingana na taarifa, Trump anadaiwa alihusika na malipo ya dola za Marekani 130,000 kumnyamazisha mcheza filamu za ngono Stormy Daniels kabla ya uchaguzi kumnyamazisha kuhusu madai yake ya kufanya mapenzi usiku mmoja na Trump muongo mmoja uliopita. Trump ameendelea kukanusha mahusiano ya kingono lakini siyo malipo yaliyofanywa..

Zaidi ya hilo, upande wa mashtaka unadai kuwa kuwa ushawishi wa Trump, washiriki wa kisiasa katika shirika la American Media Inc., wachapishaji wa gazeti la biashara National Enquirer, walilipa dola 150,000 kwa Karen McDougal, Jarida la Playboy 1998 Playmate toleo la mwaka, kununua madai ya maelezo yake mwanamke huyo yaliyoandikwa humo kwamba alikuwa na mahusiano ya kimapenzi kwa mwezi mzima na Trump mwaka 2006 na 2007 na baadae kuiondoa makala hiyo isichapishwe. Trump pia amekanusha madai ya McDougal kuwa alikuwa na mahusiano ya kimapenzi naye.

Rais wa zamani wa Marekani Trump afunguliwa mashtaka na jopo la mahakama ya Manhattan, Jijini New York.
Rais wa zamani wa Marekani Trump afunguliwa mashtaka na jopo la mahakama ya Manhattan, Jijini New York.

Baada ya Trump kufikishwa mahakamani kwa mashtaka hayo, mwendesha mashtaka Bragg alisema Trump alihusika katika mradi wa “kukamata na kutokomeza” katika gazeti la udaku kununua na kukandamiza habari hasi kuhusu yeye kabla ya uchaguzi uliokuwa mbele yake mwaka 2016 “ili imsaidie Bw Trump nafasi yake ya kushinda uchaguzi.”

Waraka wenye taarifa zilizothibitishwa ulioambatana na mashtaka pia ulidai kuwa gazeti la udaku lililipa dola 30,000 kwa mlinzi wa mlangoni wa Jengo la Trump Tower, makazi na ofisi ya rais wa zamani huko New York, kukandamiza madai kuwa Trump alikuwa akimhudumia mtoto wa nje ya ndoa, ambapo baadae gazeti hilo liligundua kuwa siyo kweli.

Trump, mawakili wake na Warepublikan wengi wamekosoa kuwa Bragg, mwendesha mashtaka aliyechaguliwa na Wademokrat, anajihusisha na “kumtafuta mchawi kisiasa.” Mmoja wa mawakili wa Trump, katika maelezo mafupi baada ya kesi kusikilizwa, alisema mashtaka hayo yanaonyesha kuwa utawala wa sheria “umekufa” nchini Marekani.

Saa kadhaa baada ya kufikishwa mahakamani huko katika Jiji la New York, Trump aliwaambia watu waliokusanyika nje ya makazi yake binafsi ya kifahari huko Mar-a-Lago katika jimbo la Florida kwamba “mimi sikudhani kitu chochote kama hiki kinaweza kutokea Marekani.”

Rais wa zamani aliongeza: “ Uhalifu pekee niliyoufanya ni kuitetea nchi yangu bila ya uoga dhidi ya wale wanaotaka kuiangamiza.

Bragg ni lazima ashtakiwe kwa kuvujisha nyaraka za jopo la mahakama au chini ya hapo ajiuzulu, alisema Trump kuhusu mwendesha mashtaka wa wilaya ya Manhattan ambaye aliwasilisha takriban darzeni tatu za makosa ya uhalifu mkubwa dhidi yake, Trump akisema kesi hiyo imeletwa kuingilia kati uchaguzi wa urais wa mwaka 2024.

Imeandikwa na mwandishi wa VOA, Ken Bredemeier, Washington, DC

XS
SM
MD
LG