Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Novemba 06, 2024 Local time: 04:57

Trump afunguliwa mashtaka na jopo kuu la mahakama ya Manhattan New York


Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump
Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump

Donald Trump amefunguliwa mashtaka na jopo kuu la mahakama ya wilaya ya Manhattan katika jimbo la New York baada ya uchunguzi kuhusu pesa haramu anazodaiwa kulipwa nyota wa filamu za ngono Storm Daniels, gazeti la New York Times limeripoti Alhamisi.

Amekuwa rais wa zamani wa Marekani wa kwanza kukabiliwa na mashtaka ya uhalifu wakati ambapo anagombea tena urais mwaka ujao.

Mashtaka hayo, yaliyotokana na uchunguzi ulioongozwa na mwanasheria mdemocrat wa wilaya ya Manhattan Alvin Bragg, yanaweza kubadili mwelekeo wa kinyang’anyiro cha urais cha mwaka wa 2024.

Awali, Trump alisema kwamba angeendelea kufanya kampeni za uchaguzi wa kumteua mgombea atakayekiwakilisha chama cha Republican ikiwa angeshtakiwa kwa uhalifu.

Jopo kuu la mahakama ya Manhattan lililoitishwa na Bragg mwezi Januari lilianza kusikiliza ushahidi kuhusu jukumu la Trump katika malipo ya Daniels siku chache kabla ya uchaguzi wa rais wa 2016 ambao aliishia kushinda.

Daniels, mwigizaji na muongozaji maarufu wa filamu za ngono ambaye jina lake halisi ni Stephanie Clifford, alisema alipokea pesa hizo ili asifichuwi kitendo cha ngono alichofanya na Trump mwaka wa 2006. Trump anakabiliwa pia na kesi nyingine mbili za uchunguzi wa uhalifu. Trump amekosoa vikali hatua hiyo ya kumfunglia mashtaka, akidai imechochewa kisiasa.

XS
SM
MD
LG