Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 22, 2025 Local time: 18:42

Rais wa zamani wa Marekani atarajiwa kukamatwa rasmi na kufikishwa mahakamani Jumanne


FILE PHOTO: Rais wa zamani wa Marekani akiwa katika kampeni huko mjini Waco, Texas.
FILE PHOTO: Rais wa zamani wa Marekani akiwa katika kampeni huko mjini Waco, Texas.

Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump anatarajiwa kukamatwa rasmi na kufikishwa mahakamani Jumanne, ikiwa mara ya kwanza kwa kiongozi wa zamani wa White House kukabiliwa na mashtaka ya uhalifu.

Katika hatua isiyo ya kawaida ya historia ya Marekani, jopo la mahakama huko New York lilipiga kura Alhamisi iliyopita kumshtaki Trump kwa mashtaka yanayohusiana na kumlipa mcheza filamu za ngono wakati wa kampeni yake ya urais 2016.

Mashtaka hayo yanayosubiriwa kwa shauku kubwa yanakuja wakati Trump anataka kurejea White House baada ya kushindwa kinyang’anyiro cha kuchaguliwa tena 2020, na kumfanya ni rais pekea, wa hivi sasa au wa zamani, na pia mgombea urais pekee, kufunguliwa mashtaka.

Mashtaka hayo bado yako katika bahasha, na haiko bayana ni uhalifu gani au ni makosa ya jinai mangapi ambayo Trump ameshtakiwa. Kituo cha televisheni cha CNN kimeripoti kuwa rais wa zamani amefunguliwa mashtaka zaidi ya 30. VOA haikuweza kuthibitisha ripoti hiyo.

Katika taarifa yake, Ofisi ya Mwendesha Mashtaka wa Wilaya ya Manhattan Alvin Bragg imesema imewasiliana na wakili wa Trump “kuratibu kujisalimisha kwake katika Ofisi ya Mwendesha Mashtaka Manhattan kwa ajili ya kufikishwa mahakamani kuhusiana na mashtaka yaliyofunguliwa Mahakama ya Juu.”

Ili kujisalimisha mwenyewe, Trump, ambaye anaishi Florida, itambidi asafiri kwenda New York, atakuwa pamoja na walinjzi wa Secret Service.

Wakati akiwa achina ya ulinzi, atachukuliwa alama za vidole na kupigwa picha kabla ya kufikishwa mbele ya jaji na kuachiliwa kwa dhamana.

Vituo kadhaa vya habari, vilitaja vyanzo bila ya majina, vikisema Trump ana mipango ya kusafiri kwa ndege kwenda New York Jumatatu na kukaa usiku huo katika Jumba la Trump kabla ya kutokea mahakamani Jumanne.

Siku ya Ijumaa, maafisa wanaomlinda Trump wa Secret Service na Idara ya Polisi ya New York walitembelea jengo la mahakama ambapo Trump amepangiwa kufikishwa hapo na wakajadili mipango ya usalama.

Susan Necheles, wakili wa Trump, ameliambia shirika la habari la Reuters kuwa rais wa zamani hatakubali makosa.

“Siogopi kile ambacho kitatokea,” Trump alisema katika barua ya kuitisha michango Ijumaa.

Kampeni ya Trump imetumia kufunguliwa kwake mashtaka katika juhudi za kuchangisha fedha na kusema ilichangisha zaidi ya dola milioni 4 katika saa 24 za mwanzo baada ya kutangazwa kufunguliwa kwake mashtaka.

Baadhi ya taarifa katika ripoti hii zinatokana na mashirika ya habari ya AP na Reuters.

XS
SM
MD
LG