Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 06:57

Rais Biden amelihutubia taifa akiliomba bunge kuidhinisha sheria kudhibiti vifo vya bunduki


Rais wa Marekani Joe Biden akilihutubia taifa Alhamis na kuliomba bunge kuidhinisha sheria zitakazodhibiti vifo vya bunduki
Rais wa Marekani Joe Biden akilihutubia taifa Alhamis na kuliomba bunge kuidhinisha sheria zitakazodhibiti vifo vya bunduki

Rais wa Marekani Joe Biden ametoa hotuba huko White House alhamis usiku kwa kulitaka bunge kuidhinisha sheria za kawaida ili kujaribu kuzuia matukio ya hivi karibuni ya vifo vinavyotokana na ufyatuaji risasi wa umma ambavyo vimewashtua wamarekani wengi.

White House imesema Biden alitoa wito wa masharti mapya ili kukabiliana na janga la ghasia za bunduki ambazo zinasababisha vifo kila siku.

Haikuwa wazi kama Biden atatetea masharti yoyote maalum ambavyo angependelea yapitishwe, kama vile ukaguzi unaoangalia historia ya nyuma kwa wanunuzi wa bunduki, au kupiga marufuku uuzaji wa silaha zenye nguvu ya haraka, ambazo zilikuwa zimetumika katika ufyatuaji risasi wa umma wa hivi karibuni.

Hakuna kipengele chochote kitakachoweza kupitishwa katika bunge lililogawanyika kisiasa ambapo wabunge kwa miaka mingi wamekuwa wakitofautiana kuhusu sheria ya kumiliki bunduki.

Lakini baadhi ya wabunge wanajaribu kuweka masharti zaidi baada ya kesi tatu za ufyatuaji risasi wa umma ndani ya kipindi cha mwezi mmoja uliopita.

Watu weusi 10 kwenye duka la vyakula waliuawa kwa kupigwa risasi katika shambulizi la ubaguzi wa rangi kwenye mji wa Buffalo katika jimbo la New York, wanafunzi 19 na waalimu wawili waliuawa kwa risasi wakiwa darasani mwao katika shule ya msingi ya Robb kwenye mji wa Uvalde katika jimbo la Texas, na watu wanne wengine waliuawa katika kituo cha matibabu cha Tulsa katika jimbo la Oklahoma.

XS
SM
MD
LG