Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 19:20

Shambulizi la mjini Tulsa labaini umuhimu wa wanunuzi wa silaha kuchunguzwa


FILE - Katika picha hii ya March 15, 2020, watu wakisubiri kuingia katika duka linalouza bunduki mjini Culver, California, Marekani.
FILE - Katika picha hii ya March 15, 2020, watu wakisubiri kuingia katika duka linalouza bunduki mjini Culver, California, Marekani.

Alipohukumiwa kwa mauaji ya vijana watatu na kumjeruhi vibaya kijana mwingine katika tafrija iliyofanyika katika nyumba moja kaskazini mwa Seattle, Allen Ivanov alisema anajuta na hawezi hata kuelezea kwa nini alifanya hilo.

Lakini aligusia sababu moja ambayo ilimuwezesha kufanya shambulizi hilo – “ni wepesi wa kupata bunduki.”

Kijana huyo akiwa na umri wa miaka 19 wakati huo alinunua silaha nzito ya kivita wiki moja kabla na alikuwa hana uzoefu wa kuitumia silaha hiyo na hivyo alikaa ndani ya gari yake nje ya tafrija hiyo na kusoma maelekezo ya namna ya kuitumia yaliyoko katika muongozo wa silaha kwa mmiliki kabla ya kufyatua risasi kumpiga mpenzi wake wa zamani na wengine.

Maelezo hayo yamejirudia tena, katika shambulizi la halaiki la hivi karibuni – huko Buffalo, New York; Uvalde, Texas; na Tulsa, Oklahoma – ambayo yaliuwa watu 35 chini ya kipindi cha wiki tatu.

FILE - kundi la walimju kutoka Dilley, Texas, wakiomboleza mauaji ya shule ya msingi Uvalde, Texas, June 3, 2022.
FILE - kundi la walimju kutoka Dilley, Texas, wakiomboleza mauaji ya shule ya msingi Uvalde, Texas, June 3, 2022.

Maelezo hayo yanaurejesha tena mjadala iwapo masharti ya uuzaji wa silaha kama vile kuweka muda wa kusubiri na kupiga marufuku ununuzi wa silaha aina ya semiautomatic kwa vijana huenda unaweza kuokoa maisha.

“Iwapo masharti hayo yangekuwepo, ingeleta tofauti kubwa,” alisema Paul Kramer, ambaye aliongoza juhudi zilizokuwa na mafanikio mwaka 2018 kuwepo kipindi cha siku 10 cha kusubiri unaponunua bunduki aina ya semiautomatic katika jimbo la Washington, hivyo hivyo marufuku kwa vijana wadogo kununua silaha kama hizo, baada ya mtoto wake Will kujeruhiwa vibaya katika shambulizi alilolifanya Ivanov miaka miwili kabla.

“Mashambulizi kama hayo ya bunduki yasingetokea namna yalivyofanyika, na kuna uwezekano mkubwa, na hivyo watu wengi wangenusurika.

Ni majimbo tisa na Washington, D.C., ambayo yanaelezea kuhusu utaratibu wa kipindi cha kusubiri kabla watu hawajanunua angalau aina fulani za bunduki.

Masharti hayo yanaweza kuipa mamlaka muda zaidi wa kufanya uchunguzi wa historia ya mnunuzi wa silaha, na kuhakikisha watu wenye kukurupuka na hamasa kuweza kumiliki silaha ambazo wangeweza kuzitumia kujiuwa au kuwauwa wengine, kulingana na Kituo cha Kisheria cha Giffords cha Kuzuiaa Ghasia za Bunduki

Serikali kuu haijaweka muda wa kusubiri. Mswaada uliopitishwa na Baraza la Wawakilishi la Marekani linaloongozwa na Wademokrat mwaka jana utaongeza muda wa kupitia historia ya mnunuzi wa silaha kutoka siku tatu hadi 10.

Lakini hilo linapingwa na Warepublikan na siyo sehemu ya mazungumzo ya hivi sasa katika Baraza la Seneti jinsi bunge linavyoweza kujibu mauaji yaliyotokea hivi karibuni.

XS
SM
MD
LG