Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Novemba 05, 2024 Local time: 14:25

Biden anakwenda kuhani familia za waathirika wa mauaji ya wanafunzi, waalimu


Rais Joe Biden na mkewe Jill Biden wakielekea kupanda ndege ya Rais Air Force One huko katika Kituo cha Jeshi la Anga cha Jeshi la Kitaifa, New Castle Delaware, Jumapili May 29, 2022, kuelekea ziara ya Ulvade. (AP Photo/Evan Vucci)
Rais Joe Biden na mkewe Jill Biden wakielekea kupanda ndege ya Rais Air Force One huko katika Kituo cha Jeshi la Anga cha Jeshi la Kitaifa, New Castle Delaware, Jumapili May 29, 2022, kuelekea ziara ya Ulvade. (AP Photo/Evan Vucci)

Rais wa Marekani Joe Biden Jumapili anakwenda  Uvalde, katika mji  uliopo kwenye jimbo la kusini magharibi la Texas, Marekani, ikiwa ni mara ya pili mwezi huu anakwenda katika mji ambao umeshuhudia shambulizi la bunduki.

Wanafunzi 19 na walimu wawili waliuawa wiki iliyopita mjini Uvalde wakati kijana mwenye silaha alipovamia shule ya msingi na kufyatua risasi.

Mapema mwezi huu, Biden alikwenda Buffalo, New York, ambako mzungu mwenye itikadi kali za ubaguzi alipofyatua risasi katika duka moja, na kuwauwa watu Weusi 10.

Jumapili akiwa Uvalde, Biden, atafuatana na mkewe Jill Biden, atakutana na familia za waathirika hao na walionusurika katika shambulizi hilo shuleni. Pia watatembelea eneo la kumbukumbu lililotengwa kwa ajili ya waathirika hao na kuhudhuria ibada katika Kanisa Katoliki la Sacred Heart.

Jumamosi huko Uvalde, darzeni ya watu walikusanyika kuomboleza na kuwakumbuka watu 21 waliouawa.

Misalaba 21 imewekwa kuzunguka eneo la mapambo lenye maji ya chemchemi katika uwanja wa mahakama ya jiji hilo, kila mmoja kwa ajili wanafunzi 19 wa darasa la nne waliofariki na walimu wao wawili, Irma Garcia na Eva Mireles.

Maua yanazidi kuongezeka, sanamu za wanyama na ujumbe kadhaa – “tunawapenda,” “Tutawakosa” – ikizunguka misalaba hiyo. Darzeni ya mishumaa ikiwaka mfano wa mwanga wa milele.

Mchungaji Humberto Renovato, miaka 33, anayeishi Uvalde, alimtaka kila mtu kushikana mikono na kusali.

Uchunguzi uliendelea Jumamosi kuhusu muda polisi waliochukua kumkabili mtu huyo mwenye silaha, Salvador Ramos mwenye umri wa miaka 18.

Kiasi cha dakika 90 zilipita tangu alipogonga gari aina ya pickup ndani ya shimo karibu na shule hiyo na alipigwa risasi na kuuawa na maafisa wa doria wa mpakani.

Mtu huyo aliyekuwa na silaha aina ya AR-15-style Rifle na begi lililokuwa na risasi, alikuwa shuleni hapo kwa dakika 40 hadi saa moja kabla ya maafisa wa polisi kuwasili na kumuua.

Baadhi ya taarifa katika habari hii inatokana na vyombo vya habari The Associated Press and Reuters.

XS
SM
MD
LG