Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 22:49

Wamilliki wa bunduki Marekani wafanya mkutano wao Texas


Makau makuu ya chama cha wamiliki bunduki Marekani mjini Fairfax, Virginia.
Makau makuu ya chama cha wamiliki bunduki Marekani mjini Fairfax, Virginia.

Chama cha Kitaifa cha wamiliki bunduki nchini Marekani kinaendelea na kongamano lake, la kila mwaka Ijumaa mjini Houston, jimbo la Texas.

Mkutano kikao hicho kimekuja siku chache tu baada ya kijana mmoja mwenye bunduki kuingia katika shule ya Msingi katika mji wa Uvalde, katika jimbo hilo, na kuua watoto 19 na walimu wawili. Gavana wa Texas Gregg Abbott, ambaye alitarajiawa kutoa hotuba ya moja kwa moja kwenye kongamano Ijumaa, amejiondoa kwa ratiba hiyo, na badala yake atazuru mji wa Uvalde, na kuhutubia kongamano hilo kwa njia ya mtandao.

Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump, hata hivyo, bado alitarajiwa kuzungumza katika hafla hiyo ya siku tatu, ya kundi la kutetea haki za bunduki.Wakati huo huo, mamlaka ya kutekeleza sheria ya Texas inakabiliwa na maswali magumu kuhusu muda uliochukuliwa kabla ya maafisa wa usalama kufika katika shule ya msingi ya Robb, kukabiliana na mvamizi huyo, Salvador Ramos.

Shambulizi hilo la shule ya msingi ya Robb, katika mji wenye idadi kubwa ya jamii ya Kilatino, linaingia katika rekodi mbaya zaidi baada ya lile la mauaji ya watoto 20 na watu wazima 6, katika shule nyingine ya msingi ya Sandy Hook, ya Newtown, Connectcut hapo Desemba 2012.

XS
SM
MD
LG