Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 16:23

Watu 15 wauawa katika shambulio kwenye shule ya msingi katika jimbo la Texas


Polisi wakitembea karibu na shule ya msingi ya Robb kufuatia shambulio la risasi, May 24, Uvalde Texas. Picha ya AP.
Polisi wakitembea karibu na shule ya msingi ya Robb kufuatia shambulio la risasi, May 24, Uvalde Texas. Picha ya AP.

Gavana wa jimbo la Texas Greg Abbot anasema watu 15 waliuawa Jumanne katika shambulio la risasi kwenye shule moja ya msingi.

Abbot anasema mshukiwa wa shambulio hilo, kijana mwenye umri wa miaka 18, amefariki pia na anaaminika kuuawa na maafisa wa usalama.

Anasema watoto wa shule 14 na mwalimu wao waliuawa jana Jumanne kwenye shule ya msingi ya Robb huko Uvalde, umbali wa maili 85 kutoka mji wa San Antonio.

Shambulio hilo la Texas linajiri chini ya wiki mbili baada ya mwanaume mzungu mwenye umri wa miaka 18 kufyatua risasi kwenye duka la chakula mjini Buffalo jimbo la New York na kuua Wamarekani weusi 10, shambulio ambalo lilitajwa na maafisa kuwa la chuki ya ubaguzi.

XS
SM
MD
LG