Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 23:16

Rais Biden anasisitiza bunge kupitisha sheria mpya ya udhibiti wa bunduki Marekani


Rais Biden na mkewe Jill Biden walipotembelea shule ya msingi Robb kutoa heshima kwa waathirika wa tukio la ufyatuaji risasi
Rais Biden na mkewe Jill Biden walipotembelea shule ya msingi Robb kutoa heshima kwa waathirika wa tukio la ufyatuaji risasi

Rais wa Marekani Joe Biden alisema Jumatatu kwamba ufyatuaji risasi wa umma nchini Marekani umekuwa mbaya sana kwamba hata wale wanaopinga masharti kwa mauzo ya bunduki wamekuwa na busara zaidi katika kujaribu kuzuia ghasia.

Siku moja baada ya ziara yake yenye hisia katika shule ya msingi ya Robb kwenye jimbo la Texas ambako mtu mwenye silaha wiki iliyopita aliua watoto 19 na waalimu wawili katika shule hiyo.

Rais Biden alisisitiza tena msukumo wake kulitaka bunge kupitisha sheria mpya ya udhibiti wa bunduki ikiwezekana kupanua ukaguzi zaidi wa historia kwa wanunuzi wa bunduki kabla ya mauzo kukamilika na hatua nyingine mbadala.

Maseneta wakuu wa Democratic ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakishinikiza udhibiti mkali katika umiliki wa bunduki wanasema wabunge wa Republican ambao takribani kwa pamoja wanapinga masharti zaidi kama ukiukaji wa uhuru binafsi wanashiriki katika majadiliano mazito kuhusu hatua gani mpya zinaweza kupata idhini ya bunge hata hivyo mabadiliko yanaweza kuwa ya kawaida.

XS
SM
MD
LG