Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 09:49

Waathirika wa mauaji Texas waashiria kuishitaki kampuni ya Daniel Defense


Vibanda vya chakula, mashine za kuuza bidhaa na meza zimewekwa katika eneo la yadi 40 ambapo kampuni ya Daniel Defense ilikuwa iweke kibanda chake katika mkutano wa mwaka wa Chama cha Taifa cha wamiliki wa silaha Marekani (NRA), Houston convention center, May 27, 2022.
Vibanda vya chakula, mashine za kuuza bidhaa na meza zimewekwa katika eneo la yadi 40 ambapo kampuni ya Daniel Defense ilikuwa iweke kibanda chake katika mkutano wa mwaka wa Chama cha Taifa cha wamiliki wa silaha Marekani (NRA), Houston convention center, May 27, 2022.

Baba wa binti wa miaka 10 aliyeuawa huko Uvalde, Texas, katika shambulizi la bunduki na mfanyakazi  mmoja wa shule wamechukua hatua za awali ambazo zinaweza kupelekea mashtaka dhidi ya  Daniel Defense, mtengenezaji wa bunduki zilizotumika kushambulia na kuwaua watu 21.

Mawakili wa Alfred Garza, baba wa mwanafunzi wa Shule ya Msingi ya Robb Amerie Jo Garza, aliomba katika barua yake Ijumaa kwamba kampuni ya Daniel Defense itoe taarifa kuhusu utangazaji wa biashara yake kwa vijana na watoto

“Tunawataka muanze kutoa taarifa kwetu hivi sasa, badala ya kumlazimu Bwana Garza afungue kesi ili kupata taarifa hizo,” ilieleza barua hiyo.

Hakuna kesi iliyotangazwa kufunguliwa hadi hivi sasa dhidi ya Daniel Defense kutokana na mauaji hayo.

Daniel Defense ya huko Black Creek, Georgia, haikujibu haraka ombi la kutoa maoni yao.

Mtu huyo aliyekuwa na bunduki kutoka Uvalde, Salvador Ramos, 18, aliivamia shule hiyo hapo Mei 24 na kuua wanafunzi 19 na walimu wawili kabla ya kuuawa na maafisa wa polisi, kwa mujibu wa maafisa.

Aliinunua kisheria bunduki ya kwanza wakati wa sikukuu yake ya kuzaliwa kwake Mei 17.

Kesi ya Sandy Hook

Josh Koskoff, Wakili wa Garza, aliongoza kesi ya shambulizi la bunduki la msingi ya Sandy Hook huko Newtown, Connecticut, mwaka 2012, ambayo ilipelekea maridhiano ya malipo ya dola milioni 73 yaliyofanywa na mtengenezaji bunduki Remington mwezi Februari.

FILE — Mzazi akiondoka na mtoto wake kutoka Shule ya Msingi ya Sandy Hook baada ya shambulizi la bunduki shuleni mjini Newtown, Connecticut, Disemba 14, 2022. (Frank Becerra Jr./The Journal News via AP)
FILE — Mzazi akiondoka na mtoto wake kutoka Shule ya Msingi ya Sandy Hook baada ya shambulizi la bunduki shuleni mjini Newtown, Connecticut, Disemba 14, 2022. (Frank Becerra Jr./The Journal News via AP)

Hii ilikuwa ni hatua ya kwanza muhimu ya maridhiano dhidi ya mtengenezaji silaha katika kesi ya mauaji ya watu wengi; kampuni kama hizo zinalindwa na sheria ya serikali kuu kushtakiwa.

“Maamuzi ya Sandy Hook huko Connecticut hayailazimishi mahakama ya Texas kuyafuata lakini hiyo haina maana uamuzi huo hauna ushawishi wa kisheria,” Koskoff alisema.

Koskoff ameiambia Reuters alikuwa anatumia kile alichojifunza kutokana na kesi ya Sandy Hook katika uchunguzi wake wa hivi sasa, akijikita katika utangazaji wa biashara hiyo kwa watoto na vijana na kuwekwa kwa bidhaa hiyo katika mchezo wa video unaotumia silaha.

“Mshamnbuliaji huyo, kimsingi siku aliyofikia umri wa miaka 18, alifahamu fika ni aina gani ya silaha alikuwa ananunua,” Koskoff alisema.

Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la Reuters

XS
SM
MD
LG