Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 20:40

Maandamano ya 'March for Our Lives' yarejea na shinikizo la udhibiti wa bunduki


Wafanyakazi wakiandaa maandamano ya "March for Our Lives" katika eneo la National Mall, karibu na White House, Washington, June 10, 2022.
Wafanyakazi wakiandaa maandamano ya "March for Our Lives" katika eneo la National Mall, karibu na White House, Washington, June 10, 2022.

Wakiwa wamekasirishwa na idadi kubwa ya mauaji kutokana na uhalifu wa kutumia bunduki, maelfu ya watu wanatarajiwa kukusanyika sehemu mbalimbali wikiendi hii.

Mikusanyiko hii itakuwa katika mji mkuu wa taifa hili na sehemu nyingine nchini Marekani ikishinikiza kuwa Bunge la Marekani lipitishe mabadiliko muhimu ya sheria za umiliki wa bunduki.

Mkusanyiko wa pili wa “March for Our Live” (tuandamane kwa ajili ya uhai wetu) utafanyika Jumamosi mbele ya eneo la Washington Monument, ikiwa ni muendelezo wa maandamano yaliokuwa yameandaliwa na waandamanaji wanafunzi March 2018 baada ya mauaji ya halaiki katika shule ya sekondari huko Parkland, Florida.

Hivi sasa kufuatia mashambulizi yaliyotokea Uvalde, Texas, hadi Buffalo, New York, na kurejesha suala la udhibiti wa bunduki katika mjadala wa kitaifa, waandaaji wa tukio la wikiendi hii wanasema huu ni wakati muafaka kurejesha tena shinikizo la mabadiliko makubwa kitaifa.

“Hivi sasa tumeghadhibika,” alisema Mariah Cooley, “mwanachama wa bodi ya “March for Our Lives” na akiwa katika mwaka wa mwisho kwenye Chuo Kikuu cha Howard.

“Maandamano haya ni kuonyesha kuwa sisi kama Wamarekani, hatutaacha kuandamana wakati wowote hivi karibuni mpaka Bunge la Marekani litakapofanya kazi yake. Na kama halijafanya hivyo, tutapiga kura kuwaondoa madarakani.”

Takriban washiriki 50,000 wanatarajiwa kujitokeza Washington DC, licha ya utabiri wa hali ya hewa kuonyesha kutakuwa na mvua.

Kwa hivi sasa ni washiriki wachache kuliko maandamano ya awali, ambayo yalileta katikati ya mji wa Washington zaidi ya watu 200,000. Safari hii, waandaaji wanajikita katika kufanya maandamano madogomadogo katika maeneo 300.

XS
SM
MD
LG