Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Novemba 05, 2024 Local time: 17:46

Ligi ya Mpira wa Kikapu Afrika msimu wa pili yaanza Jumamosi Senegal


Timu ya Morocco yaandaliwa na kocha Muaustralia
please wait

No media source currently available

0:00 0:04:21 0:00

Timu ya Morocco yaandaliwa na kocha Muaustralia

Msimu wa pili wa Ligi ya Mpira wa Kikapu ya Afrika, BAL, unaanza rasmi Jumamosi huko Dakar, Senegal, huku dazeni ya klabu za timu za wanaume kutoka nchi nyingi za Afrika vinawania taji la BAL 2022.

Klabu ya Senegal Dakar Universite na Seydou Legacy Athletique ya Guinea wanakabiliana katika mechi ya ufunguzi. Macho yao yatakuwa kwa taji ambalo liko kwa bingwa wa mwaka jana Zamalek ya Misri katika msimu wa kwanza wa BAL.

Janga la Covid 19 lilichelewesha tarehe ya awali ya mwaka 2020 ya BAL kwa mwaka mzima na masharti kuhusu michezo yake kwa wiki mbili katika mji mkuu wa Rwanda. Msimu huu michezo 38 inatarajiwa kuchezwa katika kipindi cha zaidi ya miezi mitatu miongoni mwa mechi hizo zitafanyika huko Dakar, Kigali na Cairo.

Timu za BAL zimegawanywa katika makundi mawili: Sahara na Nile. Timu za Sahara ni kutoka Guinea, Morocco, Msumbiji, Rwanda, Senegal na Tunisia—zitashinda kila mmoja mpaka Machi 15 katika uwanja wa Dakar Arena.

Timu za Nile – kutoka Angola, Cameroon, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Misri, Afrika Kusini na Sudan Kusini – zitamenyana kuanzia April 9 mpaka 19 huko katika uwanja wa ndani wa michezo wa Mostafa Hassan mjini Cairo. Kila michuano itakuwa na timu nne ambazo zitafuzu kucheza katika kutafuta mshindi wa mwisho, huku michuano ya mtoano na fainali zitakuwa katika Kigali Arena kuanzia May 21 mpaka 28.

BAL ni mpango wa pamoja kati ya NBA na Shirikisho la Kimataifa la Basketball (FIBA). Inawakilisha ushirikiano wa kwanza wa BAL kuendesha ligi nje ya Amerika.

“NBA inawekeza katika kukuza mchezo huo kote katika bara hilo, kwa upana,” Rais wa NBA Afrika, Victor William alisema, katika tukio la mwezi Februari kusherehekea ufunguzi wa ofisi mpya mjini Lagos, Nigeria. Ofisi yake ya asili ilifunguliwa Johannesburg mwaka 2010.

Timu za Ligi ya Mpira wa Kikapu
Timu za Ligi ya Mpira wa Kikapu

Afisa wa FIBA alisema kuwa msimu huu wa pili wa BAL huenda “ukapanua upeo wake na thamani ya burudani kwa mchezo huu” zaidi ya uzinduzi wa msimu wa wiki huko Kigali.

“Nchi zote Afrika zitajionea binafsi michezo hiyo,” Sam Ahmedu, rais wa FIBA Zone 3 Afrika ameiambia VOA. “...Itasaidia pia kuutangaza mchezo na kuvutia ufadhili zaidi.”

Miongoni mwa wale wanaounga mkono BAL ni makampuni kama vile NIke, Pepsi, Hennessy Cognac na RwandAir.

Taasisi mama ya BAL, NBA Afrika, imekuwa na washirika wa kimkakati kama vile rais wa zamani Barack Obama na wawekezaji ni pamoja na nyota wa zamani wa NBA Dikembe Mutombo, kiasili anatokea Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Wakati kandanda ndiyo imetawala mchezo ambao umetawala katika bara hilo, mtizamo kwa mpira wa vikapu umekuwa ukiongezeka. CNBC iliripoti kuwa lengo la NBA ni kuufanya mchezo huo uwe wa juu katika bara hilo ndani ya muongo mmoja, wakilenga zaidi vijana barani humo na jamii ya watu inayoongezeka.

Afrika ina idadi ya watu vijana zaidi duniani, huku 70% kati ya hao walio barani Afrika chini ya Jangwa la Sahara wana umri wa chini ya miaka 30, Umoja wa Mataifa umeripoti.

Msimu huu, kila timu ya BAL itatarajia jambo moja kutoka NBA Academy Afrika, kituo cha mafunzo cha mchezo wa basketball huko Saly, Senegal, kwa ajili ya watarajiwa wa juu wanafunzi wa shule. Ni kupitia programu mpya inayoitwa BAL Elevate.

“Kuna ushirikiano wa kiasili kati ya BAL na NBA Academy Afrika, na program hii itafungua njia nyingine kwa matarajio ya wasomi wa Kiafrika kufikia uwezo wao kama wachezaji na watu,” Amadoi Gallo Fall, rais wa BAL, alisema katika taarifa kwa vyombo vya habari.

Mkondo wa vipaji?

Hivi sasa, NBA ina zaidi ya wachezaji ambao ama walizaliwa Afrika au wana mzazi mmoja Muafrika, kwa mujibu wa mwakilishi wa BAL.

Wachezaji hao ni MVP mara mbili Giannis Antetokoumpo wa Milwaukee Bucks, alilelewa Ugiriki na wazazi kutoka Nigeria; Joel Embiid wa Philadelphia 76ers na Pascal Siakam wa Toronto Raptors, wote wazaliwa wa Cameroon; na Neemias Queta wa Sacramento Kings, ambaye wazazi wake wanatokea Guinea-Bissau.

Baadhi wanaona juhudi kama zile za BAL au program ya Basketball Without Borders kama ndiyo njia ya kuingia NBA. Ligi ya mwaka jana ilishuhudia NBA ikichukua wachezaji 12 au wawakilishi wa timu, Meneja wa Raptors’ Sarah Chana, aliiambia VOA wakati huo.

Lakini wapenzi wa mchezo huo kama Relton Booysen wanaona ni vyema BAL ivune na kuwalea na kuwaweka wachezaji wenye vipaji katika bara hilo.

“Kwa maoni yangu ni kwamba BAL ni tuzo. Ni tuzo kwa yeyote huko Afrika, katika dunia, kucheza kwenye BAL,” alisema Booysen, kocha mkuu wa Cape Town Tigers, timu ya Afrika Kusini, ambayo inaingia mara ya kwanza katika ligi hii hapo April 10 mjini Cairo dhidi ya klabu ya Pedro de la Rionda ya Angola. “Siyo kama unataka kutumia BAL ili kupeleka wachezaji kwa ajili ya NBA.....Naamini kwamba BAL itakuwa kubwa kama NBA.”

Mchezo wa Mpira wa Kikapu ni Utamaduni wa Kidiplomasia

Scott Brooks, mwana sosholojia na mkurugenzi mwenza wa Chuo Kikuu cha Arizona katika taasisi ya Global Sport, alisema anaziona juhudi kama za BAL kama aina fulani ya utamaduni wa Kidiplomasia. “Hii ni aina ya fulani ya jumuiya ya ulimwengu wakati unapozungumza kuhusu basketball,” alisema.

“Siyo tu utamaduni wa Kimarekani ambao unaingia. Siku zote tunapata aina za tamaduni nyingine,:” Brooks aliongeza. “Hicho ndiyo kinatia hamasa kubwa.”

Brooks alipongeza program kama vile Basketball Without Borders, NBA na za FIBA za jumuiya ya maendeleo ya ulimwengu na program uhamasishaji ili kulea wachezaji chipukizi – siyo tu katika michezo lakini pia katika masomo, afya na maadili.

“Siyo tu kuwanjega wana michezo, ni kuwajenga viongozi huko AFrika,” amesema Brooks, ambaye pia alimpongeza Fall, rais wa BAL, kwa kuwa na jukumu kubwa katika maendeleo kama haya. “Mtizamo wake siyo tu katika kucheza basketball,” Brooks alisema, lakini “wanajifunza kujitolea... na wanarudi kwenye bara hilo na kusaidia kulijenga.”

Timu zinazoshiriki zina matumaini kuwa mashindano ya BAL yataongeza upeo na misaada.

Kwa mfano, Rwanda Energy Group (REG), ambayo ilifuzu kwa msimu huu wa mashindano, haijulikani sana kwa mkazi wa Kigali Jean de Dieu Rukundo. “Siijui REG, lakini hata hivyo naiombea mafanikio,” aliiambia VOA.

Mratibu wa michezo wa REG, Geoffrey Zawadi, alielezea imani yake kwa kupata mashabiki wapya. Alisema klabu hiyo yenye miaka mitano tayari imeshinda makombe mawili ya kitaifa na “mashabiki wengi wanaongezeka kila mwaka.”

VOA kwa msimu wa pili inashirikiana na BAL, michezo 31 itatangazwa kote kwenye mitandao ya radio huko Afrika. Hiyo inajumuisha michezo maalum ambayo itatangazwa kwa ligha ya Kiingereza, Kifaransa, Kireno, Kinyarwanda na Wolof. Kilicho kipya mwaka huu, VOA na BAL wanashirikiana kwa kuwa na program za ziada ikiwemo matangazo ya podcast kila wiki kutoka Dakar, Cairo na Kigali ambayo yatarushwa hewani kupitia safu za mitandao za VOA na BAL. michezo itarushwa mubashara kupitia NBA.com na TheBAl.com.

Makala hii chanzo chake ni Kitengo cha Afrika cha Sauti ya Amerika. Wachangiaji ni pamoja na: Joad Jose Santarita, Idhaa ya Kireno; Edward Rwema, Idhaa ya Afrika ya Kati; Yacouba Ouedraoga na Tresor Matondo, Idhaa ya Kifaransa kwa Afrika; na Mike Mbonye, Idhaa ya Kiingereza kwa Afrika.

Zinazohusiana

XS
SM
MD
LG