Katika kipindi cha wiki mbili zilizopita, Zamalek na US Monastir walijipambanua kwa kuzifunga kila timu ya Ligi ya Mpira wa Kikapu ya Afrika (BAL) waliokabiliana nayo.
Zamalek na US Monastir zimefikia mchezo wa Fainali bila ya kufungwa kwa pointi 5-0 kila mmoja.
Hii ni mara ya kwanza kwa shirikisho la mpira wa kikapu Afrika kushirikiana na shirka la mpira wa kikapu la marekani NBA kuanda mchauo huu ulifanyika kwa kipindi cha wiki mbili huko Kigali.
Zamalek na US Monastir haziwajawahi kuficha malengo yao ya kushinda kombe la mwaka huu la BAL.
Timu hizo mbili zimefanya matayarisho yao kwa kuandaa wachezaji wenye ushindani na vipaji, na baada ya michezo 24 yenye dhamira ya ushindani, ni salama kusema kuwa timu hizo mbili bora zinastahili kufikia nafasi ya juu muhimu ya michuano hiyo ya msimu.
Kuweza kufikia fainali kubwa, Zamalek iliibwaga mabingwa wa championi ya Afrika kwa mara mbili Petro de Luanda kwa pointi 89-71 katika nusu fainali ya kwanza Jumamosi. Baadae, US Monastir iliwapangua machapioni wa Rwanda Patriots BBC kwa pointi 87-46.
Mechi ya Jumapili kati ya Zamalek na US Monastir siyo tu itaipa ubingwa mojawapo ya timu hizo kwa mara ya kwanza katika Ligi ya BAL, lakini pia itafungua ukurasa mpya katika historia ya mpira wa kikapu Afrika.
Lengo moja wapo la BAL kuanda mashindano hayo ni kuufanya mchezo wa mpira wa kikapu Afrika kua ni wa wachezaji wa kulipwa na Kigali ndiyo mahali inapoanzia.