Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 23:28

Kimbunga Kenneth chasitisha shughuli Comoros


Ramani ya Comoros
Ramani ya Comoros

Serikali ya Comoros, Jumatano, imefunga shule zote katika kisiwa kikubwa cha Ngazija pamoja na viwanja vya ndege na ofisi za serikali.

Kisiwa hicho cha Comoros kinatarajia kimbunga Kenneth kupita kaskazini mwa eneo la nchi hiyo huku kikitarajiwa kuwa na upepo mkali unaokwenda kwa kasi, kilometa 200 kwa saa.

Kimbunga hicho kinatarajiwa kuongezeka nguvu wakati kitakapoelekea katika pwani ya Afrika Mashariki karibu na mpaka wa Msumbiji na Tanzania.

Kimbunga hiki kinakuja wakati Msumbiji, Malawi na Zimbabwe zikiendelea kukabiliana na maafa waliyopata kutoka kimbunga Idai kilichosababisha maafa makubwa mwezi Machi.

Msemaji wa shirika la kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa, UNICEF nchini Msumbiji Daniel Timme ameiambia sauti ya amerika kwamba mashirika ya huduma za dharura yako tayari.

Pia anasema kuwa pamoja na kimbunga hiki kutokuwa na nguvu kama kile cha Idai lakini kinaelekea katika jimbo la Cabo Delgado ambako sehemu kubwa ya wakazi wake ni watu wa kipato ya chini na hawana matayarisho ya kukabiliana nacho.

Imetayarishwa na Mwandishi wetu, Abdushakur Aboud, Washington, DC.

XS
SM
MD
LG