Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 18:24

Kimbunga Fiona chaonyesha dalili za kuongeza nguvu kufikia daraja la tatu


Gari lililozama kufuatia mafuriko yaliyosababishwa na Kimbunga Fiona huko Salinas, Puerto Rico, Sept. 19, 2022.
Gari lililozama kufuatia mafuriko yaliyosababishwa na Kimbunga Fiona huko Salinas, Puerto Rico, Sept. 19, 2022.

Kimbunga Fiona kinachoongeza kasi kimeelekea kwenye visiwa vya Turks na Caicos Jumanne huku kikitishia kuongeza nguvu kufikia kimbunga daraja la tatu, kilichosababisha serikali kukataza watu kutoka nje.

Watabiri wa hali ya hewa walisema Fiona inaweza kugeuka kuwa kimbunga kikubwa ifikapo Jumatatu au Jumanne, ambapo kinatarajiwa kupita karibu na ardhi hizo za Uingereza.

“Vimbunga havitabiriki,” Waziri Mkuu Washington Misick alisema katika taarifa akiwa London, ambako alikuwa alihudhuria mazishi ya Malkia Elizabeth II. “Kwa hivyo ni lazima kuchukua kila aina ya tahadhari kuhakikisha usalama wako.”

Misick alikuwa amepangiwa kurejea nyumbani Alhamisi.

Fiona ilikuwa inapita maili 80 (kilomita 130) kusini mashariki ya Kisiwa cha Grand Turk jioni Jumatatu, Kilikuwa na upepo wenye kasi ya juu kabisa ya maili 110 kwa saa (kilomita 175 kwa saa) na kilikuwa kinaelekea kaskazini - kaskazini magharibi kwa kasi ya maili 10 kwa saa (kilomita 17 kwa saa).

Kimbunga hicho kinachoongeza nguvu kilikuwa kimeleta mvua katika Jamhuri ya Dominican na Puerto Rico, ambako mwanaume mwenye umri wa miaka 58 alifariki kufuatia taarifa za polisi kuwa alichukuliwa na maji ya mto katika mji wa kati ulioko kilimani wa Comerio.

Wakazi walioathiriwa na Kimbunga Fiona wakipumzika katiak shule moja inayotumiwa kama makazi ya muda huko Salinas, Puerto Rico, Sept. 19, 2022.
Wakazi walioathiriwa na Kimbunga Fiona wakipumzika katiak shule moja inayotumiwa kama makazi ya muda huko Salinas, Puerto Rico, Sept. 19, 2022.

Kifo kingine kilihusishwa na kukatika umeme – mwanaume mwenye miaka 70 ambaye aliungua hadi kufa baada ya kujaribu kujaza jenereta lake petroli wakati likiwa linatumika, maafisa wamesema.

Jeshi la Taifa limewaokoa zaidi ya watu 900 huku mafuriko yakiendelea kupita katika miji huko kusini na kaskazini ya Puerto Rico mvua ikifikia inchi 30 (sentimita 76) iliyotabiriwa kwa baadhi ya maeneo. Pia kumekuwa na maporomoko ya udongo kadhaa yaliorepotiwa.

Athari za Fiona zimefanya hali ya Puerto Rico kuwa mbaya zaidi kwa sababu bado ilikuwa inaendelea kukabiliana na athari za Kimbunga Maria, ambacho kiliuwa takriban watu 3,000 na kuharibu njia za umeme mwaka 2017. Miaka mitano baadae, zaidi ya nyumba 3,000 katika kisiwa hicho bado zimefunikwa na maturubali ya blue.

Maafisa wanasema takriban watu 1,300 na Wanyama 250 wa nyumbani wako katika makazi maalum ya uangalizi wa wanyama wa nyumbani kote katika kisiwa hicho.

XS
SM
MD
LG