Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 26, 2024 Local time: 09:12

Kim Jong Un alitaka jeshi kufanya matayarisho ya vita


Kombora la masafa marefu ambalo Korea Kaskazini inafanya majaribio kwa kufatua upande wa baharini.
Kombora la masafa marefu ambalo Korea Kaskazini inafanya majaribio kwa kufatua upande wa baharini.

Korea Kaskazini Ijumaa imeongeza uchokozi wa majaribio ya silaha kwa kufyatua makombora ya masafa marefu baharini, huku kiongozi Kim Jong Un akilitaka jeshi lake kufanya matayarisho ya vita wakati akitembelea kiwanda cha meli.

Wakuu wa Muungano wa Wafanyakazi wa Jeshi la Korea Kusini walisema majeshi ya Marekani na Korea Kusini walikuwa wanachambua majaribio ya silaha ya Korea Kaskazini ndani ya bahari upande wa magharibi. Ilisema jeshi la Kusini lilibaini makombora kadhaa lakini haikutoa mara moja idadi maalum au tathmini ya tabia ya urukaji wa makombora haya.

Majaribio ya makombora ya masafa marefu, yaliyofanywa na Kaskazini ya nne mwaka huu 2024, yamekuja saa kadhaa baada ya shirika la habari la serikali kuripoti kuwa Kim alirejea kulenga katika kuimarisha majeshi yake ya majini wakati alipokagua miradi ya jeshi la majini ambayo haijaelezwa katika kiwanda cha kujenga meli huko Nampho, katika pwani ya magharibi.

Kim Jong Un
Kim Jong Un

Kim katika miezi ya karibuni amesisitiza juhudi zake za kujenga jeshi la majini lenye silaha za nyuklia kukabiliana na kile anacho kionyesha kuwa kuongezeka kwa vitisho kutoka nje ya nchi vinavyofanywa na Marekani, Korea Kusini na Japan, ambao wameimarisha ushirikiano wao wa kijeshi kukabiliana na programu za silaha na makombora ya nyuklia za Kim.

Shirika rasmi la Habari la Korea Kaskazini halikueleza lini Kim alitembelea Nampho. Lilieleza Kim amesema kuwa kuimarishwa kwa jeshi lake la majini “linakuwa ni moja ya masuala muhimu kabisa kwa kulinda uhuru wa bahari kwa nchi na kuanza kujiandaa kivita.”

KCNA haikueleza ni aina gani za manowari za kivita zinazojengwa huko Nampho, lakini alisema ilikuwa inahusiana na mpango wa maendeleo ya kijeshi wa miaka mitano uliowekwa na mikutano ya chama tawala mapema mwaka 2021.

Wakati wa mikutano hiyo, Kim alitoa orodha pana ya matakwa yao ya vifaa vya kisasa vya kijeshi, ikiwemo nyambizi zinazoendeshwa na nishati ya nyuklia na makombora ya nyuklia ambayo yanaweza kurushwa kutoka chini ya maji.

Wakati wa ukaguzi huo, Kim alipewa maelezo ya maendeleo ya miradi ya jeshi la majini na baadhi ya changamoto za teknolojia na kuwaamuru wafanyakazi “bila masharti” kukamilisha juhudi hizo katika muda wa uliowekwa ambao utaendelea hadi mwaka 2025, KCNA ilisema.

Forum

XS
SM
MD
LG