Amezungumza hayo akielezea utayari wa kivita ili kukabiliana na hatua za kichokozi za Marekani vimeripoti vyombo vya habari vya serekali Jumapili.
Kauli za kiongozi huyo amezitoa wakati wa mkutano wa chama cha wafanyakazi ambacho kilijiwekea malengo kwa mwaka huu mpya na kueleza kuongeza majaribo ya silaha kabla ya uchaguzi wa Novemba wa Marekani.
Waangalizi wanasema Kim anaamini katika kuongeza uwezo wa silaha za nyuklia na kumpatia fursa nyingine kubwa ya kidiplomasia na Marekani, ilia pate ahueni ya vikwazo kama rais wa zamani wa Marekani, Donald Trump atarejea madarakani.
Forum