Kombora hilo lilirushwa kuelekea baharini katika pwani ya mashariki ya Korea Kaskazini, kwa mujibu wa mnadhimu wa jeshi la Kusini.
Takriban dakika 20 baada ya kuripoti majaribio hayo, jeshi la ulinzi la ufukweni la Japan limesema kuwa kombora lilianguka. Iliangukia eneo la kipekee la kiuchumi la Japan (EEZ), shirika la utangazaji la NTV limeripoti.
Hakuna maelezo zaidi yaliyotolewa mara moja. Majaribio hayo yamefanyika baada ya onyo kutoka kwa maafisa wa Seoul na Tokyo kwamba Korea Kaskazini yenye silaha za nyuklia inajiandaa kufanya majaribio ya makombora, ikiwa ni pamoja na moja ya makombora yake ya masafa marefu ya kwa mwezi huu.
Forum