Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 26, 2024 Local time: 21:28

Korea Kaskazini yadaiwa kuwa na makombora ya nyuklia hivi karibuni


Wachambuzi wanasema majaribio ya mkombora ya Hwasong-18 ya wiki hii ya Korea Kaskazini, yanaonyesha taifa hilo muda si mrefu litakuwa na uwezo wa kuwa na kombora la masafa marefu la nyuklia litakaloweza kufika Marekani.

Kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong Un, Jumatatu alisema kwamba majaribio ya makombora yenye nguvu ya ICBM, yameonyesha uwezo wa taifa hilo wa kuwa na makombora ya nyuklia.

Katika ripoti ya shirika la habari linalo endeshwa na serekali, Alhamisi ameongeza kusema kwamba Pyongyang, haitasita kurudisha mashambulizi endapo itachokozwa.

Hapo Jumatano, ndege za kivita za Marekani, B-1B, na Korea Kusini pamoja na Japan, zilifanya mazoezi ya anga ya pamoja katika kisiwa cha Korea Kusini, cha Jeju, katika kile mnadhimu wa jeshi hilo la pamoja alielezea kuwa ni kuonyesha nguvu katika kukabiliana na majaribio ya makombora ya ICBM.

Forum

XS
SM
MD
LG