Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Novemba 24, 2024 Local time: 01:49

Kiongozi wa Korea Kaskazini ahamasisha upanuzi wa uzalishaji mfumo wa kurushia makombora


TOPSHOT - Picha hii imepigwa Disemba 31, 2023 na kutolewa na Shirika rasmi la habari la Korea Kaskazini (KCNA) kupitia KNS on Januari 1, 2024 inaonyesha kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un (wapili kulia ) akiwa na mtotot wake.
TOPSHOT - Picha hii imepigwa Disemba 31, 2023 na kutolewa na Shirika rasmi la habari la Korea Kaskazini (KCNA) kupitia KNS on Januari 1, 2024 inaonyesha kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un (wapili kulia ) akiwa na mtotot wake.

Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un ametoa wito wa upanuzi wa  uzalishaji mfumo wa  kurushia makombora, hatua ambayo amesema  inahitajika kuchukuliwa “kwa mapambano ya kijeshi” na Korea Kusini na Marekani, vyombo vya habari vya serikali vimeripoti Ijumaa.

Taarifa ya Kim imekuja saa chache baada ya Washington kusema Korea Kaskazini iliipatia Russia makombora ya balistiki na mifumo ya kurushia makombora ambayo Russia iliyatumia hivi karibuni kushambulia miji kadhaa ya Ukraine.

Shirika rasmi la habari la Korea Kaskazini lilionyesha picha za Kim na mtoto wake wa kike, Ju Ae, wakitembelea kiwanda cha kutengeneza magari yanayobeba mfumo wa kurusha makombora, ambako aliamuru “juhudi za nguvu kuboresha uzalishaji” wa silaha hizo.

Marekani na Korea Kusini wameishutumu Korea Kaskazini kwa kuwapa Russia vifaa vya kijeshi kwa mabadilishano ya msaada wa kiufundi ili kuboresha uwezo wa kijeshi wa Korea Kaskazini. Korea Kaskazini imekanusha shutuma hizo.

Msemaji wa Baraza la Taifa la Usalama, White House John Kirby alisema Alhamisi kuwa Marekani ilikuwa na taarifa kuwa Russia imetumia mfumo wa kurusha makombora na makombora ya balistiki yaliyotolewa na Korea Kaskazini kufanya mashambulizi dhidi ya Ukraine ndani ya wiki iliyopita.

Baadaye Ijumaa, Korea Kaskazini ilirusha makombora 200 nje ya pwani ya magharibi kuelekea kisiwa cha Korea Kusini cha Yeonpyeong.

Hatua za Korea Kaskazini “zilisababisha uharibifu kwa watu wetu au jeshi,” Wakuu wa Wafanyakazi wa majeshi walisema, “lakini inatishia amani katika peninsula ya Korea na kuongeza mivutano.”

Kusini iliita hatua hiyo “ni kitendo cha uchokozi.”

Wakazi wa kisiwa hicho waliambiwa watafute hifadhi kisiwani humo wakati jeshi likijitayarisha kufanya mazoezi ya kijeshi kwa kutumia silaha za moto.

Ni ripoti ya Fern Robinson wa VOA

Forum

XS
SM
MD
LG