Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 26, 2024 Local time: 19:01

Makombora ya Korea Kaskazini yadaiwa kutumiwa na Russia, nchini Ukraine


Korea Kaskazini hivi karibuni ilipeleka makombora ya masafa ya  mbali na mifumo ya kurushia kwa Russia, ili kutumika katika vita vyake dhidi ya Ukraine, ikulu ya Marekani, imesema Alhamisi.

“Hili ni suala muhimu na linaongezeka wasiwasi,” msemaji wa Baraza la Usalama la Taifa, John Kirby, aliwaambia waandishi wa habari, akibainisha kuwa Marekani itazungumzia suala hilo katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

Akinukuu taarifa mpya za kijasusi, Kirby amesema vikosi vya Russia, vilirusha moja ya makombora yaliyotolewa na Korea Kaskazini Desemba 30, ambayo yalitua katika uwanja wa wazi katika eneo la Zaporizhzhia, Ukraine.

Amesema Russia, pia ilirusha makombora mengi ya masafa ya mbali kwenda Ukraine, kama sehemu ya shambulizi kubwa la anga Jumanne, moja ya mashambulizi makubwa zaidi katika vita ambayo vinakaribia kutimiza miaka miwili.

Forum

XS
SM
MD
LG