Uamuzi uliochukuliwa na Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan ni hatua muhimu kuelekea uanachama wa Sweden na kupunguza mivutano huko Vilnius, mji mkuu wa Lithuania. Makubaliano yalifikiwa baada ya mikutano ya siku kadhaa, na yalitarajiwa kupanua nguvu ya muungano huo huko Ulaya Kaskazini.
Katika ufunguzi wa mkutano wa NATO, katibu mkuu wa muungano huo Jens Stoltenberg alimkaribisha Rais wa Finland, Sauli Niinisto, ambaye kwa mara ya kwanza nchi yake inahudhuria ikiwa mwanachama kamili wa muungano huo.
Stoltenberg pia alitazamia Sweden nayo pia itapewa ridhaa ya kuwa mwanachama.
“Kufuatia makubaliano kutoka kwa Uturuki jana, haraka tutaikaribisha Sweden kama mwanachama kamili. Kwahiyo karibu sana. Leo, tutafanya maamuzi mengi kwa muungano huu wenye nguvu. Tutaongeza uungaji mkono hali na wa kisiasa kwa Ukraine. Hii itaileta karibu Ukraine kwa NATO ambako inatakiwa iwepo. Pia tutachukua hatua za kijasiri kuimarisha kuwweka uzio wa kukzuia, ikiwa ni pamoja na mipango mipya na majeshi kwa ulinzi wa eneo la Ulaya na Atlantiki. Tutakubaliana kuhusu ahadi ya uwekezaji katika ulinzi,” alisema Stoltenberg.
Rais wa Marekani Joe Biden alipongeza uongozi wa Stoltenberg katika NATO akisema kwamba “hakuna anayefahamu hali tunayokabiliana nayo vizuri zaidi kuliko wewe,” na kuongezea.
Rais Biden amsema, “nadhani kwa kweli ni muhimu katika wakati huu nchini Ukraine, suala zima la NATO, kwamba katibu Mkuu Jens Stoltenbrg anaendelea kuingoza NATO. Unaaminiwa. Hakuna anayefahamu hali ambayo tunakabiliana nayo vizuri zaidi kuliko wewe. Huu ni wakati wa kihistoria na kuziongeza Finland na Sweden kwenye NATO ni matokeo na kwa kweli ni suala la uongozi wako. Tunakubaliana kuhusu lugha ambayo umeipendekeza inayofanana na mustakbali wa Ukraine kuweza kujiunga na NATO.”
Mshauri wa Taifa wa Usalama wa Marekani, Jake Sullivan Jumanne alisema rais wa Marekani Joe Biden atatumia “fursa hii” kuzungumza na rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy pembeni ya mkutano wa NATO huko Vilinius.
Sullivan alisema kuendelea kwa uungaji mkono wa Mareknai kijeshi na kiuchumi kwa Kyiv katika vita vyake na Russia, pamoja na mageuzi ya kidemokrasia, yatakuwa ni miongoni mwa mada zitakazojadiliwa wakati wawili hao watakapokutana Jumatano.
“Kama Rais Biden na Rais Zelenskyy wako katika mji mmoja, watakutana tu. Marekani imekuwa muungaji mkono mkuu wa Ukraine na kumsaidia Rais Zelenskyy na watu wa Ukraine kwa utetezi wao wa kishujaa katika nchi yao na kuweza kuratibu masuala mbali mbali, msaada wetu wa kijeshi, msaada wetu wa kiuchumi, na kuendelea kufanya kazi katika mageuzi ya kidemokrasia huko Kyiv, Rais Biden atatumia fursa hiyo kuanya mazungumzo ya kina na Rais Zelenskyy kuhusu masuala hayo,” Jake Sullivan amesema.
Mkutano huo unatarajiwa kuidhinisha mipango ya kina ya kwanza ya NATO tangu kumalizika kwa vita baridi na kujilinda na shambulizi lolote kutoka Russia.
Moscow, ambayo imeielezea NATO kuhusu upanuzi wake wa mashariki kama kigezo kikuu katika uamuzi wa kuivamia Ukraine, ameukosoa mkutano huo wa siku mbili.
Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la AP.
Forum