Katibu Mkuu wa NATO, Jens Stoltenberg amesema Jumatatu kwamba Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amekubali kutuma itifaki ya Sweden kujiunga na NATO kwa Bunge la Uturuki haraka iwezekanavyo na kusaidia kuhakikisha kuwa bunge hilo linaidhinisha.
Stoltenberg alitoa tangazo hilo baada ya mazungumzo na Erdogan na Waziri Mkuu wa Sweden, Ulf Kristersson katika mkesha wa mkutano wa NATO nchini Lithuania. Hatua ya Sweden kujiunga na NATO imekuwa ikikabiliwa na pingamizi kutoka Uturuki tangu mwaka jana.
Hii ni siku ya kihistoria, kwa sababu tuna dhamira ya wazi ya Uturuki kuwasilisha nyaraka za kuridhia kwa Bunge Kuu la Taifa na kufanya kazi pia na bunge ili kuhakikisha linaridhia, Stoltenberg aliwaambia waandishi wa habari.
Mapema Jumatatu, wakati NATO ikitarajia kuweka hadharani umoja wake katika kuiunga mkono Ukraine zaidi ya siku 500 katika vita, Erdogan alisema atazuia njia ya Sweden kufika huko hadi wanachama wa Ulaya wa ushirika wa kijeshi ufungue njia kwa Uturuki kujiunga na kambi kubwa ya biashara duniani.
Forum