“Kwa wanajeshi wetu, maafisa wa ujasusi, walinzi wa kitaifa, walinzi wa mipaka, maafisa wa usalama, polisi wa kitaifa, maafisa wengine wote pamoja na watu wetu, nina washukuru. Ahsanteni sana kwa wale wote wanaoipigania Ukraine. Kwa hakika tutashinda.” amesema.
Rais huyo alitoa hotuba yake akiwa kwenye kisiwa cha Snake ambacho kilishambuliwa na Russia katika siku za kwanza za uvamizi, wanajeshi wake waliokuwa wakilinda bahari ya Black Sea walikaidi amri ya kujisalimisha kutoka kwa wanajeshi wa Russia.
Russia hata hivyo ilichukua udhibiti wa kisiwa hicho ambacho baadaye kilikombolewa tena na vikosi vya Ukraine. Marekani Ijumaa imetangaza kwamba itatoa silaha za mbali mbai kwa Ukraine, wakati kiongozi wa NATO akisema kwamba watazungumzia kuhusu uwezekano wa Ukraine kujiunga na muungano huo.
Hayo yatajadiliwa kwenye mkutano wa wanachama unaofanyika wiki hii nchini Lithuania.
Forum