Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 18:37

Uturuki yasita tena kuridhia Sweden kujiunga na NATO


Waziri mkuu wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan .
Waziri mkuu wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan .

Rais wa Uturuki ameashiria kwa mara nyingine tena kuwa nchi yake haiko tayari kuidhinisha uanachama wa Sweden katika muungano wa kijeshi wa NATO.

Akizungumza baada ya mkutano wa Baraza la Mawaziri Jumatatu, Recep Tayyip Erdogan, alisema ilibidi kufanya bidii zaidi ili kukithi vigezo vya kujiunga na NATO."

Uturuki inaishutumu nchi hiyo kwa kutochukua hatua zinazostahiki dhidi ya makundi ambayo Ankara inayachukulia kama tishio la usalama.

NATO inataka kuidhinisha uanachama wa Sweden wakati viongozi wa NATO watakapokutana nchini Lithuania wiki ijayo.

Uturuki na Hungary ndizo nchi pekee ambazo bado hazijaidhinisha uanachama wa Sweden.

Erdogan pia alisisitiza tena shutuma zake maandamano yaliyopelekea kuchomwa kwa Quran yaliyofanyika nchini Sweden wiki iliyopita, akielezea hatua hiyo kama "uhalifu wa chuki" dhidi ya Waislamu.

Sweden na Finland ziliacha misimamo yao yamuda mrefu ya kutoshiriki katika miungano ya kijeshi, na kutafuta ulinzi chini ya mwavuli wa usalama wa NATO, zikihofia huenda zikalengwa na Moscow baada ya Russia kuivamia Ukraine mwaka jana.

Finland ilijiunga na muungano huo mapema mwaka huu baada ya bunge la Uturuki kuridhia ombi lake.

Forum

XS
SM
MD
LG