Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Novemba 05, 2024 Local time: 22:43

Uturuki: Erdogan anakabiliwa na wakati mgumu kuimarisha uchumi baadaa ya uchaguzi mkuu


Rais wa Uturuki Tayyip Erdogan wakati akitangaza baraza lake la mawaziri mjini Ankara, Uturuki. June 3, 2023.
Rais wa Uturuki Tayyip Erdogan wakati akitangaza baraza lake la mawaziri mjini Ankara, Uturuki. June 3, 2023.

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan, ambaye alishinda mhula mwingine madarakani kwa hadi ya kuimarisha uchumi wa nchi hiyo na kupunguza gharama ya maisha, anakabiliwa na hali ngumu ya kiuchumi huku sarafu ya Uturuki ikiwa imepoteza thamani dhidi ya dola.

Lira ya Uturuki imepoteza thamani dhid ya dola kwa kiasi cha asilimia 20 tangu mwaka huu kuanza na kuongeza hofu ya kuongezeka kwa bei ya bidhaa hasa chakula.

Uturuki imekumbana na ukosefu mkubwa wa pesa, na mfumuko wa bei tangu mwaka 2021

Wataalam wa uchumi wanaamini kwamba hali hiyo imesababishwa na fikra za Erdogan kwamba kuongeza kiwango cha riba ni hatua itakayopelekea kuongezeka kwa mfumuko wa bei.

Erdogan ameshinkiza benki kuu ya Uturuki kupunguza gharama ya kupata mikopo, kinyume na hatua zingine zinazochukuliwa na benki zingine kuu duniani za kuongeza gharama ili kudhibithi bei.

Benki kuu ya Uturuki imepunguza kiwango cha riba kutoka asilimia 19 mwaka 2021 hadi asilimia 8.5 lakini mfumuko wa bei ulipanda hadi asilimia 85 mwaka uliopita.

Forum

XS
SM
MD
LG