Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 21:46

Mataifa ya kiislamu yakashifu kuchomwa kwa Quran kwenye maandamano ya Sweden


Waandamanji wa Iran wakichoma bendera ya Sweden baada ya Quran kuchomwa Sweden wakati wa maandamanaji
Waandamanji wa Iran wakichoma bendera ya Sweden baada ya Quran kuchomwa Sweden wakati wa maandamanaji

Mataifa 57 ya Kiislamu Jumapili yamesema kwamba juhudi za pamoja zinahitajika ili kuzuia kudhihakiwa kwa kitabu kitakatifu cha Quran, wakati wakiomba sheria za kimataifa kutumika kusitisha chuki za kidini, kufuatia kuchomwa kwa Quran wakati wa maandamano ya hivi karibuni nchini Sweden.

Taarifa kutoka kwa baraza la ushirikiano wa kiislamu ambalo wengi wa wanachama ni kutoka mataifa yenye wingi wa Waislamu imetolewa baada ya kikao maalum cha kuzungumzia suala hilo kumalizika mjini Jeddah Saudi Arabia, Jumatano wiki iliyopita.

Mwanaume aliyekuwa kwenye maandamano alichoma Quran nje ya msikiti uliopo katikati mwa mji wa Stockholm Jumatano ikiwa siku ya kwanza ya sherehe za Kiislamu za Eid al Adha. Tukio hilo liligadhabisha Uturuki ambayo ni mwanachama wa baraza hilo la kiislamu, na ambayo Sweden, inhitaji uungwaji mkono wake, ili kujiunga na NATO.

Polisi wa Sweden awali walikuwa wametoa kibali cha kufanyika kwa maandamano hayo, lakini baada ya tukio hilo, mhusika alikamatwa na kufunguliwa mashitaka ya kushambulia kundi la kabila fulani au la kitaifa.

Forum

XS
SM
MD
LG