Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 21:54

Erdogan ameapishwa rasmi kuendeleza utawala wa miongo 3


Rais wa Uturuki Recepp Tayyip Erdogan
Rais wa Uturuki Recepp Tayyip Erdogan

Rais wa Uturuki Recepp Tayyip Erdogan ameapishwa kwa mhula mwingine wa maika 5 madarakani, na kuendeleza utawala wake kwa muongo wa tatu.

Erdogan ameapa kulinda Uturuki, katiba, mfumo wa sheria, demokrasia na kuleta mabadiliko nchini Uturuki.

Sherehe ya kuapishwa kwake imefanyika katika bunge la Uturuki mjini Ankara na kuonyeshwa moja kwa moja na televisheni za Uturuki.

Erdogan, ambaye ameongoza Uturuki kwa muda mrefu zaidi, alipata asilimia 52.2 ya kura katika duru ya pili ya uchaguzi wa urais uliofanyika May 28.

Alishinda uchaguzi huo licha ya kuwepo mfumuko mkubwa wa bei nchini Uturuki, uliomwekea mazingira magumu kuwashawishi wapiga kura.

Forum

XS
SM
MD
LG