Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Novemba 05, 2024 Local time: 22:41

Zelenskyy aomba NATO ikubali Ukraine kujiunga baada ya vita kumalizika


Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy

Rais wa Ukraine Volodymr Zelenskyy Jumatano ameomba NATO iweke bayana kwenye kongamano litakalofanyika mwezi ujao, kwamba taifa lake linaweza kujiunga baada ya vita vyake na Russia kumalizika.

Wakati akitoa hotuba mbele ya bunge wakati wa maadhimisho ya siku kuu ya katiba ya Ukraine, Zelenskyy amesihi viongozi wa ulimwengu kutojali namna Moscow itakavyochukulia hatua hiyo, wakati akitaja viongozi wa kijeshi na kisiasa wa Russia kuwa magaidi.

Baadaye alieleza matarajio ya Kyiv wakati wa mkutano wa NATO utakaofanyika kati ya Julai 11 na 12 nchini Luthiania, muda mfupi baada ya kufanya kikao na rais wa Poland Andrzej Duda, na mwenzake wa Lithuania Gitanas Nauseda, mjini Kyiv.

Wakati akihutubia wanahabari, Zelenskyy alisema kwamba, “Tunafahamu vyema kwamba hatuwezi kujiunga na NATO wakati mapigano yakiendelea, lakini tunahitaji hakikisho kwamba hilo litafanyika baada ya vita kumalizika.”

Forum

XS
SM
MD
LG