Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 09:50

Biden akutana na Waziri Mkuu wa Sweden White House


Rais Biden akiwa na mgeni wake Waziri Mkuu wa Sweden Ulf Kritersson ikulu ya Marekani.
Rais Biden akiwa na mgeni wake Waziri Mkuu wa Sweden Ulf Kritersson ikulu ya Marekani.

Rais wa Marekani Joe Biden ni mwenyeji wa Waziri Mkuu wa Sweden Ulf Kristersson kwa mazungumzo Jumatano huko  White House wakati viongozi wa NATO wakijitayarisha kwa mkutano wa viongozi wa juu nchini Lithuania.

Sweden inajaribu kujiunga na NATO, hatua iliyochochewa na uvamizi wa Russia nchini Ukraine mwaka 2022. Viongozi wa NATO waliidhinisha uanachama wa Sweden katika mkutano wao wa mwaka 2022, lakini Uturuki na Hungary hawajaidhinisha ombi la Sweden katika mchakato ambao lazima nchi zote wanachama zipitishe uamuzi huo kwa pamoja.

Finland iliomba uanachama pamoja na Sweden na ilikubaliwa kikamilifu katika NATO mwezi Aprili.

“Rais Biden na Waziri Mkuu Kristersson watapitia masuala ya ushirikiano wa kiusalama unaoendelea kukua baina yetu na kuthibitisha tena maoni yao kuwa Sweden lazima ijiunge na NATO haraka iwezekanavyo,” msemaji wa White House Karine Jean-Pierre alisema katika taarifa yake wiki iliyopita.

Uturuki imekuwa ikiishutumu Sweden kwa kutochukua hatua kwa vikundi ambavyo Uturuki inaviona ni taasisi za kigaidi. Ikiwa ni sehemu ya makubaliano yaliyofikiwa na Uturuki, Sweden na Finland, Sweden imepitisha mageuzi kadhaa ikiwemo sheria mpya ya kupambana na ugaidi.

Katibu Mkuu wa NATO Jens Stoltenberg anapanga kuzikutanisha nchi hizo tatu pamoja kwa mazungumzo siku ya Alhamisi.

Jean- Pierre alisema Biden na Kristersson watajadili uratibu kuhusu China na pia hatua za kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa na teknolojia zinazoibuka hivi sasa.

.

Baadhi ya taarifa katika habari hii zinatokana na mashirika ya habari ya AP na Reuters.

Forum

XS
SM
MD
LG