“Majadiliano ya ukweli na yenye tija yalisaidia juhudi zinazoendelea, kuendeleza njia za wazi za mawasiliano na kuwajibika katika kusimamia mahusiano ya pande mbili ya Marekani na China,” Wizara ya Fedha ya Marekani ilieleza katika taarifa yake.
Vyombo vya habari vya China vilisema Xie alielezea matumaini yake kuwa nchi hizo mbili zitaondoa kuingiliana kati na kuimarisha mazungumzo.
Kusimamia mahusiano, kushughulikia masuala mbalimbali yenye maslahi ya pamoja na kuhakikisha mivutano haigeuki kuwa migogoro imekuwa ni mada muhimu katika mazungumzo kati ya maafisa waandamizi katika wiki za karibuni, ikiwemo ziara ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken huko Beijing mwezi uliopita.
Wizara ya Fedha ilisema katika mazungumzo yake na Xie, Yellen “aliibua masuala yanayotia wasiwasi na pia kuwasilisha umuhimu wa uchumi mkubwa kabisa wa pande mbili kushirikiana kukabiliana na changamoto za dunia, ikiwemo masuala ya mfumo mpana wa uchumi na kifedha.”
Yellen anatarajiwa kuzuru China kuanzia Julai 6-9 kwa ajili ya mazungumzo na maafisa wa ngazi ya juu.
Baadhi ya taarifa katika habari hii inatokana na mashirika ya habari ya AP, AFP na Reuters.
Forum