Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 10:31

China yatoa mwaliko kwa waziri mkuu wa Israel


Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu
Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu

Kiongozi huyo ameyasema hayo wakati akifanya kikao na wajumbe wa bunge la Marekani wanaofanya ziara nchini humo. Mwaliko huo unafuatia hatua nyingine kadhaa hapo nyuma kutoka Beijing za kuimarisha ushawishi wake wa kidiplomasia kwenye eneo hilo, na unakuja wakati kukiwa na taharuki kati ya utawala wa Marekani wa Joe Biden na serikali ya Netanyahu yenye misimamo mikali ya kiyahudi.

Ofisi ya Netanyahu imesema kwamba iwapo atakubali mwaliko huo, basi itakuwa ziara yake ya nne nchini China akiwa waziri mkuu. Imeongeza kusema kwamba tayari utawala wa Biden umefahamishwa kuhusu mwaliko huo. China katika miezi ya karibuni imekuwa ikiongoza kwenye harakati za kurejesha uhusiano wakidiplomasia mashariki ya kati , wakati ikiongoza makubaliano ya kurejesha uhusiano kati ya Israel na hasimu wake Iran, na Saudi Arabia mwezi Aprili, pamoja na kualika rais wa Palestina Mahmoud Abbas mjini Beijing mapema mwezi huu.

Forum

XS
SM
MD
LG