Hatua hiyo kwa shirika hilo la Umoja wa Mataifa lenye makao yake mjini Paris, hatua inayotarajiwa kuongeza mamilioni ya dola, pamoja na kuipa Marekani usemi kwenye program kadhaa kama vile mabadiliko ya hewa, elimu na intelijensia ya kubuni.
Wengi wanatarajia kwamba ombi hilo litakubalika wakati wa kikao maalum cha UNSECO kitakachofanyika Alhamisi na Ijumaa.Kufikia sasa hakujakuwa na pingamizi kutoka kwa mataifa yote 193 wanachama, ingawa China na Russia wametoa tahadhari kadhaa dhidi ya hatua hiyo.
Baadhi wanapendekeza kwamba Israel ambayo ilijiondoa kwenye shirika hilo inahitaji kufuata nyayo za Washington za kujiunga tena.
Forum