Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 04:27

Wanne wakamatwa China kwa kuhusika na tukio la mlipuko


Polisi wa China wamekamata watu wanne Jumamosi waliohusishwa na mlipuko katika mgahawa ambao uliua watu kadhaa, vyombo vya habari vya serikali vimeripoti.

Takriban watu 31 waliuwawa na wengine saba kujeruhiwa wakati mlipuko wa gesi ulipotokea kwenye mgahawa wa kuchoma nyama katika mji wa Yinchuan kaskazini magharibi mwa nchi siku ya Jumatano.

Ilifanyika katika mkesha wa mapumziko ya siku tatu ya tamasha la mashua ya Dragon wakati watu wengi nchini China walienda nje na kujumuika na marafiki.

Washukiwa hao ni pamoja na mmiliki wa mgahawa, wanahisa wawili na meneja, shirika la habari la serikali Xinhua limeripoti.

Walikamatwa kwa madai ya kusababisha ajali mbaya kwa uzembe na uchunguzi wa uhalifu ulikuwa unaendelea, Xinhua imesema. Ofisi ya usalama wa umma ya eneo hilo ilikuwa imezuia mali za watu tisa, wakiwemo wanne waliokamatwa, ilieleza.

Forum

XS
SM
MD
LG