Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 05:25

Rais Biden asherehekea White House Siku ya Uhuru kwa matukio mbalimbali


FILE - Rais Joe Biden akiwasalimia wananchi baada ya maonyesho ya fataki wakati wa sikukuu ya Siku ya Uhuru wa Marekani White House, Julai 4, 2022, Washington.
FILE - Rais Joe Biden akiwasalimia wananchi baada ya maonyesho ya fataki wakati wa sikukuu ya Siku ya Uhuru wa Marekani White House, Julai 4, 2022, Washington.

Rais wa Marekani Joe Biden anasherehekea sikukuu ya Siku ya Uhuru wa nchi hii kwa matukio kadhaa huko White House.

Rais na mkewe Jill Biden wanafanya sherehe wakishirikiana na Jumuiya ya Elimu ya Kitaifa, na kisha kuwakaribisha familia za wanajeshi kwa ajili ya nyama choma.

Biden amepangiwa kuzungumza jioni katika kumbukumbu ya sikukuu hii akiwa na kundi la wanajeshi na familia za wanajeshi wa zamani pamoja na wanaowasimamia huko White House.

Shughuli hiyo iliyoandaliwa na White House itatoa eneo lililo wazi kwa ajili ya kuangalia maonyesho ya urushaji fataki unaofanyika Washington katika viwanja vya National Mall.

Sherehe za sikukuu ya Siku ya Uhuru wa Marekani huko Boston, Julai 1, 2023. (AP Photo/Michael Dwyer)
Sherehe za sikukuu ya Siku ya Uhuru wa Marekani huko Boston, Julai 1, 2023. (AP Photo/Michael Dwyer)

Viwanja vya Bunge la Marekani vitakuwa ni eneo la maonyesho ya kila mwaka ya Siku ya Uhuru, tamasha hilo litaonyeshwa moja kwa moja kupitia televisheni kwa taifa.

Watakaoshiriki kutumbuiza mwaka huu ni pamoja wasanii Chicago, Babyface, Kikundi cha National Symphony Orchestra na bendi ya Jeshi la Marekani.

Washington pia ni mwenyeji wa matembezi ya kawaida ya Siku ya Uhuru katika barabara ya Constitution Jumanne.

Forum

XS
SM
MD
LG