Lakini Wamarekani Weusi wamekuwa wakiadhimisha siku hii tangu Juni 19, 1865, wakati majeshi ya Marekani yalipowasili katika jimbo la Texas kutangaza kuwa vita vimemalizika na jeshi la upinzani (Confederate) wamesalimu amri mwezi April.
Ilikuwa miezi miwili baada ya Appomattox, mji mdogo katika jimbo la Virginia nchini Marekani ambako Jenerali wa Confederate Robert E. Lee alikabidhi upanga wake akisalimu amri kwa Jenerali wa Jeshi la Marekani Ulysses S. Grant. Lakini habari za kumalizika kwa uasi zilikuwa hazijafika katika majimbo yote ya Marekani yaliyokuwa yameasi mwaka 1861.
Mnamo Juni 19, 1865, Jenerali wa Jeshi la Marekani Gordon Granger na majeshi yake yaliwasili katika pwani ya mji wa Galveston, Texas. Alipowasili, alitangaza “Amri ya Kijeshi No.3” ikitangaza kumalizika kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe, na kwa amri hiyo, ukombozi wa kiasi cha watu Weusi 250,000 waliokuwa katika utumwa kote huko Texas, sehemu ya mwisho iliyokuwa inashikilia watumwa.
“Watu wa Texas wanajulishwa kuwa, kulingana na tamko la Kiutendaji la [rais] wa Marekani, watumwa wote wako huru,” amri hiyo ilieleza.
Kuachiliwa huru watu Weusi kuliletwa na Rais Abraham Lincoln Januari 1, 1863 kwa Tamko la Kuachiliiwa Huru, lakini ilichukua muda mpaka Majimbo ya Confederate ya Marekani yalipositisha kwa amri hiyo k
Mwezi Desemba, 1865, Marekebisho ya 13 la Katiba ya Marekani yalifanyika, na kuidhinisha milele ukombozi wa watu Weusi na wengine waliokuwa katika utumwa.
“Siyo utumwa wala kufanyishwa kazi kwa nguvu, ispokuwa tu ikiwa ni adhabu kwa kosa la uhalifu kutokana na muhusika atapokuwa amepatikana na hatia, itakuwepo nchini Marekani, au sehemu ambapo sheria hizo zinatumika,” ilieleza.
Sherehe za Juneteenth zilianza huko Texas lakini zikasambaa katika maeneo mengine ya Marekani katika miaka ya baadae. Kuhamia kwa watu Weusi upande wa kaskazini kutoka majimbo yaliyokuwa yanashikilia watumwa ya kusini mwa Marekani, jamii za watu Weusi katika maeneo mengi yaliadhimisha siku hiyo kwa magwaride na sherehe nyingine mbalimbali.
Juneteenth ilipata umaarufu wakati wa miongo kadhaa ya misukosuko katika miaka ya 1950 na 1960 wakati Wamarekani Weusi walipokuwa wakidai na kupokea sheria zinazolinda haki za kuwa na makazi, kupiga kura, kuajiriwa, na mambo mengine muhimu. Umuhimu wa siku hiyo ya uhuru ambayo ni Juneteenth ilisimama imara.
Texas lilikuwa jimbo la kwanza kutambua umuhimu wa Juneteenth, kwanza kwa kutoa tamko mwaka 1938, na sheria hiyo kuanza kutumika Januari 1, 1980 ikiadhmisha Juni 19 kuwa sikukuu rasmi ya jimbo.
Majimbo mengine pia yaliadhimisha Juneteenth kwa namna fulani rasmi kwa miaka yote hii, ikifikia kilele chake Juni 17, 2021 sheria iliposainiwa na Rais Joe Biden ikiifanya June 19 kuwa sikukuu ya serikali kuu.
Juneteenth ni sikukuu rasmi ya pili ya serikali ya Marekani inayowaenzi Wamarekani Weusi. Sikukuu ya serikali kuu ya kwanza inaenzi siku ya kuzaliwa kwa mwanaharakati wa haki za kiraia na mhanga Mchungaji Dr Martin Luther King, Jr., kumkumbuka yeye na harakati na kujitolea kwa watu Weusi nchini Marekani.
Na kwa sikukuu ya Juneteenth ya pili Marekani ikiadhimishwa, mwanamke Mweusi, Kamala Harris
Wakati minyororo ya utumwa imefunguliwa kwa zaidi ya miaka 150, watetezi wa haki za walio wachache wanasema mengi lazima yafanyike kuwapa watu Weusi Marekani kiti katika meza. Wanaeleza sababu za kiuchumi na za kijamii ambazo zinaendelea kuwaweka katika fursa isiyo nzuri watu Weusi na wengine.