Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Januari 24, 2025 Local time: 00:07

Marekani yaadhimisha miaka 245 ya uhuru wake


Julai 4, inasherehekea siku ambayo mwaka 1776 wawakilishi kutoka makoloni 13 ambayo yaliungana pamoja na kuwa Marekani na walipitisha azimio la kihistoria la Uhuru kutoka kwa utawala wa Uingereza.

Siku hii ya Julai 4 imefanywa ni likizo ya kitaifa tangu mwaka wa 1941.

Kawaida ni siku kwa familia na marafiki kukusanyika pamoja, kupika na kula vyakula mbalimbali.

Miji mingi kote nchini husherehekea siku hii kwa maonyesho kwa gwaride na fataki.

Mwaka 2021 sikukuu ya uhuru inakuwa mara ya kwanza kwa familia nyingi na marafiki kuonana baada ya zaidi ya mwaka mmoja, wakati nchi inapoanza kutoka katika masharti yaliyowekwa kudhibiti janga la COVID-19.

"Tunashikilia ukweli huu kuwa dhahiri, kwamba wanaume wote wameumbwa sawa, kwamba wamejaliwa na muumba wao na haki kadhaa zinazoweza kupatikana, kwamba kati ya hizo ni maisha, uhuru na kutafuta furaha," Waasisi waanzilishi wa taifa la Marekani waliandika katika Azimio la Uhuru.

Wanawake hawakuhesabiwa kuwa sawa, na wengi wa waliyosaini tamko hilo walikuwa wamiliki wa watumwa ambao hawakuwaona watumwa kuwa sawa, au kupewa haki.

Maadhimisho hayo yanafanyika wakati bado Marekani ikiendelea kupambana na ukosefu wa usawa wa rangi na jinsia.

Chanzo cha habari : AP

XS
SM
MD
LG