Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 07:44

Watu milioni 1 wahitaji msaada wa dharura Tigray


Luteni Jenerali Bacha Debele wa Jeshi la Ulinzi la Ethiopia, kulia , akiwa na msemaji wa kikosi kazi cha Tigray, Redwan Hussein wakizungumza na waandishi wa habari juu ya hali ya mkoa wa Tigray, Addis Ababa, Ethiopia, Juni 30, 2021.
Luteni Jenerali Bacha Debele wa Jeshi la Ulinzi la Ethiopia, kulia , akiwa na msemaji wa kikosi kazi cha Tigray, Redwan Hussein wakizungumza na waandishi wa habari juu ya hali ya mkoa wa Tigray, Addis Ababa, Ethiopia, Juni 30, 2021.

Wasiwasi umeendelea kuongezeka kuhusu hali ya maisha ya watu wa jimbo la kaskazini mwa Ethiopia la Tigray.

Mapema wiki hii waasi wa Tigray waliingia kwenye mji mkuu wa jimbo hilo Mekelle.

Miezi karibu minane ya mapigano imewaacha zaidi watu milioni moja wakihitaji msaada wa dharura wa chakula kulingana na makadirio ya Umoja wa Mataifa.

Kuondolewa kwa vikosi vya serikali ya Ethiopia bado hakujabadilisha hali ya njaa kwa wale wanaohitaji chakula.

Mkuu wa shirika la wakimbizi la UN anasema kuwa hali ya kibinadamu inaendelea kuzorota.

Hata hivyo, serikali ya Ethiopia imekanusha madai kwamba inazuia misaada kufikia wanaohitaji.

Demeke Mekonnen Hassen, Naibu Waziri Mkuu wa Ethiopia na Waziri wa Mambo ya nje ameeleza haya : "Dhana kwamba tunajaribu kuwakandamiza watu wa Tigray kwa kukataa misaada ya kibinadamu kuwafikia na kutumia njaa kama silaha ya vita ni potofu. Hakuna sababu kabisa kwetu kufanya hivyo. Hawa ni watu wetu na ukweli wa mambo ni kwamba tunatumia nguvu zetu zote kuwaondoa katika hali mbaya wanayokumbana nayo kwa sasa na hilo ni jukumu letu kwa kweli. "

Naibu wake Redwan Hussien aliwaambia waandishi wa habari kwamba serikali iko tayari kuisaidia Umoja wa Mataifa kusafirisha misaada kutoka mji mkuu Addis Ababa kwenda kwenye viwanja viwili vya ndege, katika jimbo la Tigray.

Lakini ameongeza kuwa haitawajibika kwa kile kitakachotokea mara tu UN itakapowasili katika mkoa huo.

Shirika la habari la Reuters linamnukuu mratibu wa dharura wa Mpango wa Chakula Ulimwenguni wa UN akisema kuwa usafirishaji wa misaada unaweza kuanza tena na watu 40,000 wanaohitaji msaada wanaweza kufikiwa mwishoni mwa wiki hii.

XS
SM
MD
LG