Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 20:56

Ethiopia kufanya uchaguzi Jumatatu


Mtu akimbia mbele ya mabango ya wagombea kwenye uchaguzi wa Ethiopia
Mtu akimbia mbele ya mabango ya wagombea kwenye uchaguzi wa Ethiopia

Wapiga kura wa Ethiopia Jumatatu wanashiriki kwenye uchaguzi wa kitaifa na majimbo, likiwa zoezi ambalo waziri mkuu Abiy Ahmed ameeleza ni ishara ya demokrasia baada ya kuminywa kwa muda mrefu katika taifa hilo la pili kwa wingi wa watu barani Afrika.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters, Ahmed mwenye umri wa miaka 44 ameleta mabadiliko makubwa ya kisiasa nchini humo tangu kuchaguliwa mwaka 2018 kupitia muungano wa vyama tawala.

Hata hivyo baadhi ya wakosoaji wake wanasema kuwa hatua zilizopigwa huenda zijkahujumiwa kutokana na madai ya uhalifu wa kivita kwenye eneo la Tigray, suala ambalo serikali inakana.

Abiy wiki iliyopita alisema kuwa uchaguzi wa Jumatatu utakuwa jaribio la kwanza la zoezi huru na lenye haki , wakati uchumi wa taifa hilo ukiwa umeathiriwa vibaya na janga la corona.

Uchaguzi huo huenda ukaathiri mataifa ya kieneo kutokana na kuwa Ethiopia inashiriki kwenye maswala ya kidemokrasia ya kieneo kama vile kutoa walinda usalama nchini Somalia, Sudan na Sudan kusini. Chama kipya cha Abiy cha Prosperity ni miongoni ya vingine vingi vinavyoshiriki kwenye zoezi hilo.

Imetayarishwa na Harrison Kamau

XS
SM
MD
LG