Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 18:46

Ethiopia yaitisha sitisho la mapigano Tigray


Mifugo wapita karibu na kifaru kilochoharibiwa kwenye mapigano ya Tigray
Mifugo wapita karibu na kifaru kilochoharibiwa kwenye mapigano ya Tigray

Serikali ya Ethiopia Jumatatu imetangaza sitisho la mapigano katika jimbo la Tigray, miezi minane baada ya mzozo mbaya uliosababisha mafaa mengi, wakati ma elfu ya wakazi  wakikabiliwa na baa la njaa.

Sitisho hilo la mapigano huenda likatuliza hali kwenye taifa hilo la pili kwa wingi wa watu barani Afrika.

Taarifa inajiri wakati Ethiopia ikisuburi matokeo ya uchaguzi wa kitaifa ambao waziri mkuu Abiy Ahmed aliuelezea kama kiini cha mageuzi yaliyompelekea kushinda tuzo ya amani ya Nobel mwaka 2019.

Taarifa ya serekali ilitolewa na vyombo vya habari muda mfupi baada ya utawala wa mpito wa Tigray ulioteuliwa na serekali kuu kukimbia katika mji mkuu wa Tigray, Mekele, na kuomba sitisho la mapigano kwa sababu za kibinadamu ili misaada inayohitajika ifikishwe kwa kwa wakazi. Wakati huo huo, wakazi wa Mekele wameshangilia kuwasili kwa vikosi vya Tigray.

XS
SM
MD
LG