Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 14:17

Wapiganaji wa TPLF waonya kuangamiza uwezo wa vikosi vya serikali


Vikosi maalum vya Amhara vkiondoka baada ya makabiliano na TPLF kwenye picha ya awali
Vikosi maalum vya Amhara vkiondoka baada ya makabiliano na TPLF kwenye picha ya awali

Wapiganaji kutoka jimbo lililokumbwa na mzozo laTigray, Ethiopia Jumanne wameonya kwamba wanajeshi wao watatafuta mbinu za kuharibu uwezo wa vikosi vya Ethiopia na Eritrea, licha ya serikali ya Ethiopia kutangaza sitisho la mapigano la upande mmoja katika jimbo hilo.

Serikali ya Ethiopia ilitangaza sitisho la mapigano kupitia vyombo vya habari vya serekali hapo Jumatatu, na kusema kwamba litaanza kutekelezwa mara moja.

Taarifa ya sitisho hilo la mapigano imejiri baada ya miezi minane ya mzozo huko Tigray, na wakati wanajeshi wa chama tawala cha zamani katika jimbo la Tigray waliingia katika mji mkuu wa jimbo hilo, Mekelle, na kulakiwa kwa shangwe na wakazi wa mji huo.

Msemaji wa vikosi vya Tigray Jumanne ameonya katika mahojiano na shirika la habari la Reuters kwamba wanajeshi wa Tigray wataingia katika nchi jirani ya Eritrea na katika jimbo la Ethiopia la Amhara, kuvisaka vikosi adui iwapo itahitajika.

Wanahabari wa VOA kwenye mji wa Mekelle wamesema hawajaona wanajeshi wa serikali ya Ethiopia mjini humo tangu Jumapili.

XS
SM
MD
LG