Takriban watu 100, wengi wao wakiwa ni wahitimu wa jeshi, walikuwa katika ndege aina ya C-130 Hercules iliyokuwa inajaribu kutua katika kisiwa cha Jolo, kwenye jimbo la Sulu wakati wa mchana.
Baadhi ya wanajeshi walioonekana wakiruka kutoka katika ndege kabla ya kufika ardhini na kuwaka moto, amesema Meja Jenerali Williams Gonzales, kamanda wa kikosi kazi cha pamoja -Sulu.
Ilikuwa ni moja ya ajali mbaya sana za ndege ya jeshi nchini humo kuwahi kutokea.
“Hii ni siku ya kusikitisha, lakini ni lazima tuwe na matumaini,” Gonzales alisema katika taarifa yake.
“Tunaungana na taifa kuwaombea wale waliojeruhiwa na wale waliokufa katika ajali hiyo.”
Shughuli za uokoaji zinaendelea kwa watu 17 ambao hawajapatikana.
Chanzo cha Habari : AFP