Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 19:35

Upinzani waomba nafasi zaidi ya kisiasa, Tanzania


Aliyekuwa mgombea wa urais kutoka upinzani Tundu Lissu wakati wa kampeni zilizopita, Tanzania
Aliyekuwa mgombea wa urais kutoka upinzani Tundu Lissu wakati wa kampeni zilizopita, Tanzania

Viongozi wa upinzani pamoja na wanaharakati wa Tanzania Alhamisi wamefanya kikao cha kuomba serikali kufanya marekebisho kwenye katiba ili kuongeza uhuru  wa kisiasa nchini.

Kikao hicho kilichopewa jina Katiba Day, kimefanyika muda mfupi baada ya rais mpya Samia Hassan kuomba watanzania kumpa nafasi ya kufufua uchumi kwanza kabla ya kufanya marekebisho ya katiba.

Kikao cha Alhamis kinaonekana kuchochewa na matamshi ya rais Hassan hapo Jumatau wakati alipofanya kikao cha kwanza na wanahabari. Kiongozi huo aliomba watanzania kumpa nafasi ya kufufua uchumi kwanza kabla ya kuondoa marufuku iliowekwa dhidi ya mikutano ya kisiasa pamoja na kurejea mchakato uliositishwa kuelekea marekebisho ya katiba.

Kiongozi aliyemtangulia marehemu John Magufuli alisitisha mchakato wa marekebisho ya katiba muda mfupi baada ya kuchukua hatamu za uongozi mwaka wa 2015, huku akipiga marufuku mikutano yote ya kisiasa mwaka uliofuata.

Wanasiasa wa upinzani wanasema kuwa hakuna sababu yoyote ya kumpa muda zaidi rais Hassan kwa kuwa kutoa nafasi ya demokrasia hakuwezi kuathiri ukuaji wa uchumi.

Benson Singo ambaye ni naibu katibu wa chama cha upinzani cha demokrasia na maendeleo au CHADEMA alihoji ni vipi demokrasia ingezuia ukukuaji wa kiuchumi.

Makundi ya kutetea haki yanasema kuwa marekebisho ya katiba yanastahili kuwa kipaumbele cha rais kwa kuwa yanaleta udhabiti kama alivyosema Onesmo Olengurumwa ambaye ni mkurugenzi wa muungano wa watetezi wa haki za kibinadamu nchini Tanzania.

Sasa hivi Tanzania inatawaliwa na katiba ya 1977 ilioandikwa chini ya mfumo wa chama kimoja cha kisiasa. Wapinzani pamoja na wakosoaji wanasema kuwa inahitaji kufanyiwa marekebisho kwa kuwa inaegemea upande wa chama tawala cha CCM..

XS
SM
MD
LG