Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 20:18

Familia ya Martin Luther King Jr. yaomba maadhimisho ya kumbukumbu yake kuahirishwa


Martin Luther King Jr.
Martin Luther King Jr.

Jumatatu ya tatu ya kila mwezi Januari ni sikukuu ya serikali kuu kumuenzi Martin Luther King Jr., ambapo wahamasishaji wa leo wa haki za kiraia wanakabiliwa na ukweli kuwa pamoja na kuongezeka kwa mtizamo wa umma juu ya vitendo vya ubaguzi, wanaelekea katika kuona upungufu wa kushindwa kutimiza malengo yao kuboresha makundi ya walio wachache kuweza kupiga kura.

Wiki iliyopita familia ya King iliomba sherehe za urithi wa kiongozi wa haki za raia ziahirishwe mwaka huu, mpaka Bunge la Marekani litakapopitisha sheria ya kuongeza haki za kupiga kura nchini Marekani.

Wademokrat wamehamasisha sheria ambayo itaipa Washington sauti yenye nguvu jinsi uchaguzi wa serikali kuu unavyoendeshwa katika kila jimbo kati ya majimbo 50 ya Marekani.

Wakati serikali kuu haina mamlaka ya kusimamia uchaguzi katika ngazi ya jimbo, matakwa mapya ya serikali kuu yanaweza kuwaathiri, kwa sababu kwa kawaida unafanyika wakati mmoja.

Kati ya vipengele vingine, miswaada miwili iliyodhaminiwa na Wademokrat, Sheria ya Uhuru wa Kupiga Kura na Sheria ya Haki ya Juu ya Kupiga Kura ya John Lewis, inakusudia kuondoa sheria ambazo zilipitishwa na majimbo yanayoongozwa na Warepublikan wanayodhibiti njia na fursa za kupiga kura.

Wademokrat na wanaharakati wengi wa haki za kiraia wanasema sheria za jimbo zitawakandamiza wapiga kura walio wachache, na wanawatuhumu Warepublikan kwa ukandamizaji uliojificha zaidi wa kupiga kura. Warepublikan wanapinga tuhuma hizo, wakisisitiza kuwa lengo lao ni kulinda hadhi ya uchaguzi na kuepusha wizi wa kura.

Siku ya Mapumziko

Kila mwaka Wamarekani wanapumzika siku ya Jumatatu ya tatu ili kuadhimisha sikukuu ya kitaifa kukumbuka siku aliyozaliwa kiongozi mtetezi wa haki za binadamu aliyeuwawa, Martin Luther King Jr.

King alipata umaarufu mwaka wa 1955 alipoongoza mgomo wa kususia mabasi ya umma kwenye mji iliopo kusini wa Montgomery, Alabama na kupelekea kumalizika kwa ubaguzi wa rangi dhidi ya wasafiri weusi. Alikuwa kiongozi mkuu wa harakati za kupigania haki katika miaka ya 50 na 60 huku akiwapa motisha mamilioni ya watu wakati wa hotuba yake ya "I have a dream" kwenye maandamano yaliofanyika machi mwaka wa 1963 hapa mjini Washington Dc.

Aliweza kupata tuzo la Nobel mwaka uliofuata wa 1964 wakati rais Lyndon Johnson alipotia sahihi mswaada wa haki za binadadamu. King aliuwawa tarehe 4 Aprili mwaka wa 1968 huko Memphis, Tennessee alipokuwa amesafiri na kuungana na wafanyakazi weusi wa kuzoa takataka waliokuwa wamegoma wakitaka malipo sawa.

Sikukuu hii ilianza mwaka 1983 wakati rais Ronald Reagan alipotia sahihi mswaada wa kuitenga siku ya Jumatatu ya tatu ya mwezi Januari kuwa ya kumkumbuka King aliyezaliwa Januari 15 ,1929. Congress iliidhinisha sikikukuu ya King kuwa ya kitaifa mwaka 1994 kama siku ya kujitolea katika jamii.

XS
SM
MD
LG