Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 07:57

Shujaa wa kupigania haki za kiraia Marekani John Lewis afariki


Hayati John Robert Lewis
Hayati John Robert Lewis

John Robert Lewis, shujaa wa kupigania haki za kiraia kwa ajili ya Wamarekani Weusi na Mwakilishi wa muda mrefu katika Baraza la Wawakilishi Marekani, amefariki akiwa na umri wa miaka 80.

Mwakilishi huyu maarufu amefariki Ijumaa baada ya mwaka mmoja wa kupambana na saratani iliyokuwa imepevuka.

John Lewis aliibuka kuwa mashuhuri kama kiongozi wa kipindi cha sasa aliyeshiriki katika harakati za haki za kiraia miaka ya 1950 na 60.

Akiwa na umri wa miaka 23, alifanya kazi karibu sana na Mchungaji Martin Luther King, Jr. na alikuwa pekee yuko hai kama mzungumzaji mkuu wakati wa maandamano ya mwaka 1963 mjini Washington ambako King alitoa hotuba yake maarufu “I Have a Dream” (Nina Ndoto).

Wakati wa mkutano huo wa kihistoria, Lewis aliwakumbusha Wamarekani juu ya nguvu za harakati za haki za kiraia.

“Kwa nguvu ya madai yetu, ari yetu, na idadi yetu, tutaondoa ubaguzi katika eneo la Kusini na tutawaunganisha wananchi kwa nguvu za Mungu na demokrasia.

Ni lazima tuseme : “Amkeni Wamarekani! Amkeni! Kwani hatuwezi kusita, na hatutasita kamwe na hatuwezi kuvumilia tena,” alisema Lewis, akizungumza na kundi la watu 250,000.

XS
SM
MD
LG