Trump alisaini sheria ya uhuru wa Hong Kong, Jumanne, inayomruhusu kuwawekea vikwazo na marufuku ya visa maafisa wa China na mashirika mengine ya kifedha yanayo jihusisha na kuiwekea Hong Kong sheria ya usalama wa taifa.
Jarida la Bloomberg lilikuwa limeripoti rais Trump alikuwa amesitisha hatua ya kuwawekea vikwazo zaidi maafisa wa China ili kuzuia mgogoro kati ya Marekani na China.
Miongoni mwa wanaolengwa kuwekewa vikwazo ni pamoja na mkuu wa mji wa Hong Kong Carrie Lam kwa kuunga mkono utekelezaji wa sheria ya usalama.
Wiki iliyopita, Trump aliwawekea vikwazo maafisa kadhaa wa Chama cha Kikomunisti cha China - CCP, kutokana na namna walivyo wadhulumu Waislamu wa Uighur.