Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Novemba 27, 2024 Local time: 05:54

HABARI ZA DUNIA KWA UFUPI :Waziri Mkuu wa Tunisia ajiuzulu.


Waziri Mkuu wa zamani wa Tunisia Elyes Fakhfakh.
Waziri Mkuu wa zamani wa Tunisia Elyes Fakhfakh.

Waziri mkuu wa Tunisia Elyes Fakhfakh amejiuzulu Alhamisi.

Hatua hiyo inaiweka Tunisia katika mgogoro mkubwa wa kisiasa wakati inajaribu kukabiliana na athari za kiuchumi kutokana na janga la virusi vya Corona.

Serikali ya Fakhfakh inasambaratika miezi mitano baada ya kuundwa na huenda ikachelewesha mabadiliko makubwa ya kiuchumi yanayohitajika.

Inaweza pia kuathiri mipangilio iliyopo ya namna ya kukabiliana na janga la virusi vya Corona baada ya kudhibithi awamu ya kwanza ya maambukizi.

Nchi za magharibi ziliisifu Tunisia kwa mabadiliko ya uongozi kwa njia ya demokrasia tangu mwaka 2011, yalipotokea maandamano yaliyopelekea mabadiliko makubwa katika uongozi wan chi hiyo.

Lakini utafiti unaonyesha kwamba idadi kubwa ya raia wa Tunisia hawana furaha na uongozi wa sasa kutokana na uchumi mbaya, hali mbaya ya Maisha na huduma mbovu za uma huku wanasiasa wakiendelea kuweka mikakati ya ku

Mahakama Malaysia yakuza kampuni ya Saudi kutumia fedha zilizoibiwa

Mahakama nchini Malaysia Alhamisi imetoa kibali cha muda, kuzuia kampuni ya Mafuta ya PetroSaudi international, kutumia zaidi ya dola milioni 340 zilizo nchini Uingereza, ambazo waendesha mashtaka nchini Malaysia wanaamini kwamba ziliibwa kutoka katika mfuko wa maendeleao wa 1 MDB.

Maafisa wa Marekani na Malaysia wanasema kwamba karibu dola bilioni 4.5 ziliibwa kutoka kwa mfuko wa maendeleo wa Malaysia – 1 MDB, katika sakata iliyomhusisha aliyekuwa waziri mkuu wa Malayis Najib Razak na benki ya Marekani ya Goldman Sachs, miongoni mwa wat una mashirika mengine.

Najib amekana mashitaka kuhusika na sakata hilo.

Mwezi Februari, mawakili wa kampuni ya Goldman sachs, walikataa mashtaka katika mahakama ya Malaysia, ya kuwapotosha wawekezaji kuhusu uuzaji wa hisa za kiasi cha dola bilioni 6.5 ambazo benki ya uekezaji ya Marekani ilisaidia mfuko wa uekezaji wa Malaysia – 1MDM, kupata.

Kampuni ya Novartis kusaidia nchi zinazoendelea tiba dhidi ya COVID-19

Kampuni ya kutengeneza dawa ya Novartis Sandoz division, imesema kwamba itahakikisha kwamba dawa inayotengeneza ya kusaidia katika tiba dhidi ya maambukizi ya virusi vya Corona, itatolewa kwa nchi zinazoendelea, bila ya kutaka kupata faida.

Kampuni hiyo ya Uswizi, imesema kwamba itatoa dawa hiyo kwa zaidi ya nchi 79 zilizorodeshwa na benki ya dunia zenye kipato cha chini kabisa ama zenye kiwango cha wastani ngazi ya chini.

Kampuni hiyo imetangaza kwamba hailengi kupata faida yoyote kutokana na dawa hizo, hadi pale janga la virusi vya corona litakapomalizika kabisa au hadi chanjo ya corona itakapopatikana.

Mpango huo unalenga kuzisaidia nchi zenye mifumo duni ya afya katika nchi za Afrika, Asia, Amerika kusini, Ukraine na Maldova.

Kampuni ya Novartis haijapungukiwa na kiwango cha dawa inazotengeneza licha ya mahitaji kuendelea kuongezeka.

XS
SM
MD
LG